23.7 C
Dar es Salaam
Sunday, August 14, 2022

Miss Utalii yawapa semini waandishi

Brighiter Masaki -Dar es salaam

UONGOZI wa Miss Tourism Tanzania, wametoa semina elekezi kwa wahariri na waandishi wa habari ili kuwapa mafunzo ya kuandika na kuripoti habari za utalii.

Akizungumza na MTANZANIA jana wakati wa mafunzo hayo mwandaaji wa shindano hilo, Gideon Chipungahelo ‘Chips’, alisema waandishi wa habari ni watu muhimu hivyo wanapaswa kuandika mazuri kuhusu utalii.

“Unakuta mwandishi wanakosoa kwa kuandika kuwa tamasha lilidoda kweli kweli, lilihudhuliwa na watu watano bila kuangalia ana athiri vipi na baada ya shindano kuisha unaandika maisha binafsi ya kumuharibia mshindi,” alisema Chips.

Naye mwakilishi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Bona Masenge alisema mashindano ya Miss Utalii Tanzania yamejijengea umaarufu na kuweza kutangaza utalii ndani na nje ya nchi.

“Unapoona mapungufu kwenye eneo fulani  inabidi uangalie jinsi gani unaweza kuficha na kuweka heshima ya shindano, Serikali inataka kuona kupitia shindano hili tunatangaza vivutio vya Taifa letu na Utamaduni kwa ujumla,” alisema Bona Masenge

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,712FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles