24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

‘MISS U DOM’ IFUTE MADOA YANAYOICHAFUA TASNIA

NA MWANDISHI WETU

TASNIA ya urembo nchini imeendelea kukumbana na changamoto kadha wa kadha ambazo zinafanya waandaaji wa mashindano ya kusaka warembo waonekane wababaishaji na wasio na weledi katika kazi hiyo.

Matukio mengi ya kuishusha hadhi tasnia ya urembo yametokea kwa kusudi na mengine kwa bahati mbaya, kwani ni siku chache zimepita toka Miss Tanzania 2016/17 anukuliwe akilalamika kutopewa zawadi zake baada ya kushinda taji hilo kubwa la urembo nchini. Malalamiko kama hayo ni madogo, lakini yanaacha madoa kwenye ulingo wa urembo nchini.

Kiu kubwa ya mashabiki wa urembo na warembo wenyewe ni kuona wanapata shindano litakalosimamia vyema taratibu za mashindano kama hayo ili wapate zile faida zinazokusudiwa, badala ya kuishia kutangazwa washindi na kuishia mitaani.

Miongoni mwa shindano hilo, ambalo limekuwa likikua kwa kasi na kujizolea sifa kwenye ulimwengu wa urembo nchini, ni lile shindano linalowahusisha warembo wasomi wa Chuo Kikuu cha Dodoma, ambalo linatazamwa kama jiko la kupika warembo wenye viwango vya kushindana kimataifa.

Sasa msimu wa shindano hilo linalojulikana kama Miss U Dom, umefika na tayari kufanyika pale inapofika Mei 13, mwaka huu, katika ukumbi wa Royal Village, huku mgeni rasmi akiwa ni Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson, akisindikizwa na Mbunge Anthony Mavunde.

Muziki mzuri wa dansi kutoka bendi ya Twanga Pepeta utawaburudisha mashabiki wa urembo watakaohudhuria shindano hilo pale watakapotazama jukwaa lililosheheni warembo wasomi, huku wakifurahia mzaha na ucheshi wa mchekeshaji Mpoki na Dokii, watakaokuwa ma-MC.

Bila shaka tutashuhudia tofauti kubwa ya shindano la Miss U Dom na mashindano mengine ya urembo, kama anavyosema mmoja wa wadhamini wa shindano hilo anayeitwa Boss Ngassa, alipofanya mahojiano na gazeti hili.

“Historia ya Miss U Dom ni nzuri na tumedhamiria kuendelea kutoa warembo wasomi wenye sifa za kushiriki mashindano ya kimataifa, kwa hiyo wadau na mashabiki wa urembo watambue kuwa hatutawaangusha,” anasema Boss Ngassa.

Uzuri wa maandalizi ya shindano hilo hauondoi dhima na kiu ya mashabiki wa urembo kuona mashindano ya urembo yanaondokana na yale mambo yaliyoonekana kuichafua tasnia na kupaka tope majina ya wadau walioamua kuwekeza fedha zao kwenye mashindano.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles