22.2 C
Dar es Salaam
Saturday, October 1, 2022

MISS TANZANIA WAHIMIZWA KUTANGAZA UTALII

     

                                                                |Janeth Mushi, ArushaWarembo wanaoshiriki Shindano la Miss Tanzania, Kanda ya Kaskazini, wamehimizwa kutangaza utaliii wa ndani ikiwamo kuendeleza tamaduni zilizohifadhiwa katika makumbusho mbalimbali nchini.

Mkurugenzi wa Kituo cha Sanaa na Utamaduni wa Tanzania cha Cultural Heritage, Saifuddin Khanbhai amesema hayo wakati akizungumza na warembo hao walipotembelea kituo hicho.

Amesema mwitikio wa Watanzania kutembelea vivutio mbalimbali vilivyopo nchini na vile vya utamaduni ni mdogo, hivyo kuwaomba fursa waliyo nayo katika jamii kuhamasisha utalii wa ndani.

“Mwitikio wa watanzania bado ni mdogo katika kutembelea vivutio hasa vya kitamaduni, hivyo nawaomba ninyi kwa nafasi zenu katika jamii kuhamasisha utalii wa ndani, itasaidia kuongeza idadi ya watalii wa ndani na kuwajengea uzalendo zaidi wazawa na kukuza pato la taifa,” amesema.

Awali Mkurugenzi wa Kismaty Advert Media, Mary Mollel, ambao ndiyo waandaji wa shindano hilo kwa Kanda ya Kaskazini, alisema maandalizi ya shindano yako katika hatua za mwisho katika kuelekea kilele cha shindano hilo linalotarajiwa kufanyika keshi Jumamosi Julai 28, mwaka huu, katika Hoteli ya Naura Springs, jijini hapa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,373FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles