26.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 26, 2023

Contact us: [email protected]

Miss Sinza watoa msaada kwa wazazi

Miss Sinza wakielekezwa jambo walipotembelea katika ofisi za New Habari(2006) Ltd.
Miss Sinza wakielekezwa jambo walipotembelea katika ofisi za New Habari(2006) Ltd hapo jana.

THERESIA GASPER NA GLORY MLAY

MLIMBWENDE atakayeibuka mshindi kwenye shindano la Miss Sinza litakalofanyika Julai 29, Ukumbi wa Denfrance Sinza, Dar es Salaam, ataondoka na kitita cha Sh 500,000.

Mratibu wa shindano hilo, Nasib Mhinya, alisema mshindi wa pili atapata Sh 400,000 na wa tatu ataondoka na Sh 300,000 huku mshindi wa nne na watano wakipata kifuta jasho cha Sh 200,000 kila mmoja na warembo wengine watapata kifuta jasho cha Sh 100,000 kila mmoja.

Warembo hao jana walitembelea ofisi ya New Habari (2006) Ltd iliyopo Sinza Kijiweni na kujifunza mambo mengi yanayofanywa hapo kuanzia upataji wa habari hadi uchapishaji wake.

Wakati huo huo, warembo hao walitembelea Hospitali ya Palestina na kutoa zawadi mbalimbali zikiwamo sabuni kwa  mama wajawazito na wenye watoto wachanga.

Akizungumza na Gazeti hili, Ofisa Uongozi wa Hospitali hiyo, Joyce Magile, alishukuru warembo hao kwa kujitolea kwao hospitalini hapo.

“Tunashukuru sana kwa zawadi hizi mlizozitoa katika wodi hizi za wazazi wakiwemo  wajawazito na wale wenye watoto wachanga na tunaomba msiishie  hapa na mfanye na kwengine,” alieleza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,726FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles