22.7 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

Miss Dodoma yakaribisha wadhamini

Na Jeremia Ernest, Dar es Salaam

Muandaaji nguli wa shindano la Urembo jijini Dodoma, Alexander Nikitas ambaye ni Mmiliki wa kampuni ya Nikalex amewakaribisha wadau mbalimbali kujitokeza kudhamini shindano hilo mwaka huu.

Dodoma ni moja ya mikoa unaofanya vizuri katika shindano la Miss Tanzania ambapo warembo wake mara kadhaa wamekuwa wakifanya vizuri katika ngazi ya Taifa.

Akizungumza na www.mtanzania.co.tz leo Aprili 28, 2021 jijini Dodoma, Alexander amesema anakaribisha makampuni ambayo yanaweza kuungana nae kufanya shindano hilo ambalo imekuwa likiibua vipaji vya wasichana mbalimbali nchini na hivyo kuchangia kutoa ajira.

“Nichukue nafasi hii kuwaomba wadau na Serekali kuungana nami kufanikisha mchakato wa kumpata mrembo atakaye wakilisha Mkoa wetu katika shindano la taifa na kulinda heshima ya kuwa makao makuu ya nchi,” amesema Alexander.

Ameongeza kuwa tayari mchakato wa kuwapata washiriki umesha anza na mwishoni mwa Mei wanatarajia kufanya uzinduzi mkubwa kama ilivyo kawaida ya mkoa huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,283FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles