23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 8, 2023

Contact us: [email protected]

MISINGI IMARA HUJENGA FURAHA KWA FAMILIA


Na MWANDISHI WETU

BAADHI ya familia kutokana na uwezo walio nao zimeweka utaratibu wa kuishi na watu tofauti wakiwamo watoto au mfanyakazi wa nyumbani ‘house girl’.

Maisha hayo hukutanisha watu ambao wamelelewa katika mfumo fulani tofauti na familia husika.

Kutokanana na hilo, zipo changamoto lukuki zinazojitokeza hasa katika kujenga familia yenye usawa kitabia ili kuwaepusha watoto husika kutoridhi tabia mpya za kundi hilo la nje.

Miongoni mwa tabia ambazo zinasababisha usumbufu unaotokana na malezi ya hovyo ni  ni pamoja na kuingia chumba cha mtu mwingine bila kugonga hodi, kutumia kitu bila kuomba, tabia ya kufuja vitu ikiwemo chakula.

Jinsi ya kuondoa hali hiyo

Wazazi/walezi wanatakiwa kuwafundisha na kuwaelimisha watoto au watu wanaoishi nao namna wanavyotaka waishi na kuwaeleza mambo wasiyoyapenda.

Nidhamu na upendo ndilo jambo la kupewa kipaumbele.

Elezea umuhimu wa kuheshimiana, kugonga hodi kabla ya kuingia chumba cha mtu mwingine, omba ruhusa kwa kitu kinachomilikiwa na mwingine kwa ajili ya kujenga nidhamu na kutambua thamani ya mtu mwingine.

Familia inayoheshimiana siku zote ina furaha na ni nadra kuona watu wanaombeana mabaya,mama na baba wakiwa mfano mzuri basi familia nzima itaendeleza, lakini kama mama na baba wenyewe ni mgogoro hawaheshimiani wala kujali utu wa mwingine siku zote familia yao itaparaganyika.

Kama familia jengeni utaratibu wa kusameheana na kuheshimiana, ukimsamehe mwingine basi mtajenga maelewano mazuri.ieleweke kuwa sehemu yeyote yenye familia lazima kuwe na upendo, bila upendo hakuna familia.

Jengeni mawasiliano rahisi, kama familia ni vizuri mkawa na mawasiliano rahisi yasiyokuwa na mikwaruzo, zungumzeni lugha za kujenga na yakitokea malumbano basi yawe yenye kuboresha na si ya kubomoa.

Wanafamilia wanahitaji kuzungumza tena kuzungumza ukweli, uongo ni sumu ambayo inaweza kusambaratisha familia wakati wowote, ukweli huu ni lazima uanzie kwa wazazi na watu wengine watafuata, misingi hii na mingine itasaidia kuifanya familia yako kuwa na furaha wakati wote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,353FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles