MISHAHARA YA RAIS NA WABUNGE YAPUNGUZWA KENYA

0
521
3d rendered and waving flag of kenya

Tume ya mishahara na marupurupu ya watumishi wa umma nchini Kenya imetangaza kupunguzwa kwa mishahara ya maafisa wakuu wakiwemo rais na wabunge.

Mwenyekiti wa tume hiyo Bi Sarah Serem ametoa mpangilio mpya wa malipo ambao anasema utaokoa jumla ya Sh8 bilioni (dola 80 milioni za Marekani) kila mwaka na kupunguza jumla ya mishahara inayolipwa watumishi wa umma kwa asilimia 35.

Tume hiyo imependekeza kufutiliwa mbali kwa marupurupu ya kipimo cha usafiri wa magari kwa magavana na wabunge na badala yake hilo litakuwa likifidiwa na mfumo mpya wa marupurupu kwa kuzingatia kanda.

Rais sasa atakuwa akilipwa Sh1.4 milioni (dola 14,000) kila mwezi badala ya Sh1.65 milioni (dola 16,500), naye naibu wake awe akilipwa Sh1.2 milioni (dola 12,000).

Mawaziri watakuwa wakilipwa Sh924,000 (dola 9,200), Spika wa Bunge Sh1.1 milioni (dola 11,000) nao magavana wa kaunti Sh924,000 (dola 9,240).

Mabadiliko hayo yataanza kutekelezwa tarehe 8 Agosti, 2017.

Bi Serem amesema maafisa wa serikali walikuwa wakitumia vibaya mfumo wa marupurupu wa kupimiwa usafiri wa magari.

Badala yake, maafisa sasa watakuwa wakilipwa marupurupu ya kila mwezi ya usafiri kwa kutegemea eneo anamotoka afisa husika. Source BBC

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here