25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

MISHAHARA KILIO CHA TUCTA MEI MOSI

PATRICIA KIMELEMETA – Dar es Salaam


WAKATI Rais John Magufuli akitarajia kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), limesema kilio chake kwa Serikali ni kuongezwa kima cha chini cha mshahara ya watumishi wa umma na sekta binafsi.

Maadhimisho hayo yanafanyika kitaifa mjini Iringa leo.

Rais wa Tucta, Tumaini Nyamhokya, akizungumza na Mtanzania jana, alisema miongoni mwa maombi yatakayowasilishwa kwa Rais Magufuli ni nyongeza ya mishahara.

Tucta imekuwa ikipendekeza kima cha chini cha mishahara kuwa kati ya Sh 500,000 hadi Sh 750,000.

Nyamhokya alisema kima cha chini kinachotolewa hivi sasa na Serikali hakikidhi mahitaji kutokana na kupanda gharama za maisha.

“Maandalizi ya sherehe za Mei Mosi kitaifa yamekamilika, kilichobaki ni kumsubiri Rais Magufuli tuweze kuwasilisha maombi yetu ambayo pamoja na mambo mengine, wafanyakazi watataka kujua kiasi cha nyongeza ya mishahara kitakachotangazwa katika mwaka huu wa fedha 2018/19,”alisema Nyamhokya.

Alisema Serikali ilikwisha kufanya uhakiki wa watumishi hewa na wenye vyeti feki na kuwaondoa kwenye malipo, hivyo TUCTA inaamini  Serikali inaweza kuongeza mishahara ambayo itaendana na hali halisi ya maisha.

“Kima cha chini kinacholipwa hivi sasa hakiwezi kukidhi mahitaji kutokana na hali ngumu ya maisha.

“Tunaamini Serikali itaongeza mishahara kujenga morali kwa watumishi waweze kufanya kazi kwa bidii,”alisema.

Alisema nyongeza hiyo itakua chachu kwa sekta binafsi katika kuongeza mishahara kulingana na kima kitakachotangazwa na Serikali.

 

Kwa habari zaidi jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles