24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

MISAADA HAITAONDOA UMASIKINI AFRIKA – SAMIA

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, akimsikiliza Mkurugenzi wa Kampuni ya Property International, Abdul Haleem, kuhusu Ndege maalumu ya kampuni hiyo inayopiga picha za anga kwa muda mfupi wakati wa upimaji wa viwanja wakati alipotembelea banda lao kwenye Maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam jana. Na Mpigapicha Wetu.

Na ASHA BANI – Dar es Salaam

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan, amesema kutegemea misaada ya kifedha kama chanzo cha maendeleo katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) hakutasaidia kuziondolea umaskini.

Alisema badala ya kutegemea misaada hiyo, nchi za SADC zinatakiwa kutumia rasilimali za ndani kwa kushirikiana na sekta binafsi ili kuondoa utegemezi huo.

Hayo aliyasema jana Dar es Salaam, wakati wa kufungua mkutano wa nusu mwaka wa Mtandao wa Taasisi za Maendeleo ya Fedha wa Jumuiya ya Maendeleo (SADC-DFI).

“Mtakubaliana na mimi kwamba nchi nyingi za Afrika zina utajiri wa rasilimali, lakini bado masikini na watu wake masikini pia, njia ya kuutupa umasikini ni kujifunza jinsi ya kutumia taasisi za kifedha na matumizi sahihi ya miradi katika kuleta maendeleo chanya,’’ alisema Samia.

Alitoa pongezi kwa DFIs kwa kusapoti miradi ya maendeleo, ikiwa ni pamoja na ile ya muda mfupi na mrefu lengo likiwa kusaidia ukuaji wa uchumi wa viwanda.

Alisema kaulimbiu ya mwaka huu ya “Kuelekea uchumi wa viwanda kwa maendeleo endelevu na jumuishi, wajibu wa DFIs katika SADC’’, inaendana na dhamira ya Serikali ya Tanzania katika kujikita kwenye uchumi wa viwanda, hivyo ni muda mwafaka wa kutenda.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji alisema nchi za SADC zikijipanga na kutumia mabenki yake vizuri, zinaweza kupata maendeleo ya haraka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles