26.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

Miradi mitatu ya majitaka kuondoa kero Dar

Na Tunu Nassor, Dar es Salaam

Wakazi wa jiji la Dar es Salaam wanatarajiwa kunufaika na miradi mitatu mikubwa ya uchakataji majitaka inayotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasa).

Akizungumza leo Julai 12, baada ya kutembelea maeneo yanayojengwa miradi hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Dawasa, Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange amesema miradi hiyo inajengwa eneo la Jangwani, Mbezi beach na Kurasini.

Amesema kukamilika kwa miradi hiyo kutawapunguzia gharama za uondoshaji majitaka kwa wananchi ambao kwa sasa wengi wanatumia magari.

“Kwa sasa uondoshaji majitaka ni asilimia 10 lakini itakapokamilika miradi hii mitatu na ile midogo ‘off grid’ tutaweza kufikia asilimia 40,” amesema Jenerali Mwamunyange.

Amesema miradi hiyo imeanza kutekelezwa ambapo ule wa Jangwani unafanyiwa upembuzi yakinifu ili kuepuka mafuriko yanayotokea katika eneo hilo mara kwa mara.

“Mtambo unaojengwa hapa utaweza kuchakata mita za ujazo 25,000 lakini wa awamu ya pili utaweza kuchakata mita za ujazo 200,000,” amesema Mwamunyange.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles