30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Miradi 87 yaanza kutoa huduma

Na Amina Omari, Tanga

Waziri wa maji Jumaa Aweso, amesema kuwa kati ya miradi ya maji 177 ambayo ilikuwa haitoi maji, tayari  miradi 87 imeweza   kurekebishwa na kuanza kutoa huduma hiyo .

Aweso amezungumza hayo leo wakati wa hafla ya kuanza kwa ujenzi wa mradi wa kuboresha hali ya upatikanaji wa maji Tanga unaotekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (Uwasa) 

Amesema kuwa dhamira ya wizara hiyo ni kuhakikisha hadi ifikapo mwishoni mwa mwaka huu miradi yote iliyobaki ianze kutoa huduma kama ilivyokusudiwa.

“Wizara ya maji tumejipanga kuhakikisha tunatatua changamoto za upatikanaji wa maji katika maeneo yote ya mijini na vijijini kwani tayari serikali imeshatoa fedha za kutosha kuhakikisha tunamtua mama ndoo kichwani” amesema Waziri Aweso.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Tanga Uwasa, Mhandisi Geofrey Hills amesema mradi huo unatarajiwa kuongeza kiwango cha uzalishaji wa maji kutoka lita za ujazo 30, 000 hadi 45, 000 kwa siku.

“Mradi huu unatarajiwa kugharimu kiasi cha  bil 9.18 ambapo utahusisha ukarabati  na upanuzi wa mtambo wa kusafisha maji,pamoja na kulaza bomba kubwa lenye kipenyo cha milimita 600 lenye urefu wa Km 12.4” amesema Hills.

Mradi huo umepangwa kutekelezwa kwa kipindi cha miezi  15  kuanzia Agosti 2021 hadi Octoba 2022 .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles