28.6 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

Minziro: Mkataba wa ‘kisela’ umeniondoa Singida United

MOHAMED KASSSARA-DAR ES SALAAM

KOCHA Fred Minziro amefichua sababu zilizomfanya kutoonekana kwenye  benchi la timu ya Singida United,  katika michezo miwili ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, ambayo yote ilichezea vichapo.

Singida ilianza kuchapwa bao 1-0 na Mwadui FC,  katika mchezo wa kwanza  kabla ya juzi kukubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Namungo,  mchezo uliochezwa Uwanja wa Majaliwa, Lindi.

Matokeo hayo yaliibuka maswali  wapi alipo  Minziro ambaye alikabidhiwa mikoba ya kuinoa timu hiyo mwishoni mwa msimu uliopita.

Akizungumza na MTANZANIA jana , Minziro alisema ameamua kujiweka kando baada ya uongozi wa klabu hiyo kutojali mambo ya msingi,  ikiwamo kumzungusha kuhusu mkataba wa kazi.

“Baada ya kunizungusha kwa muda mrefu waliniletea  mkataba lakini haukuwa maslahi mazuri hivyo nikaamua kujiweka kando.

“Nilipousoma niliona hauna faida kwangu kwani hauna  bonsai(marupurupu), kifupi ni mkataba wa kisela, hivyo nikaona hakuna sababu ya kuusaini.

“Kwa sasa siko na timu hiyo hivyo siwezi kuzungumzia  kilichotokea kwenye michezo hiyo miwili,  uongozi hawakuthamini mchango wangu,”alisema Minziro

Minziro alifichua sababu nyingine ilimfanya kujiengua kwenye timu hiyo ni kitendo cha uongozi kujichukulia uamuzi wa kufanya usajili wa wachezaji bila kumshirikisha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles