MINAJ ATHIBITISHA KURUDI KWA NAS

0
585

NEW YORK, MAREKANI

BAADA ya mkali wa muziki wa Hip Hop nchini Marekani, Nicki Minaj kuachana na mpenzi wake Meek Mill, sasa mrembo huyo amethibitisha kurudiana na mpenzi wake wa zamani Nasir Jones ‘Nas’.

Picha za wawili hao zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii siku za hivi karibuni na kuacha maswali mengi kwa mashabiki wao, lakini mrembo huyo ameshindwa kuzuia hisia zake na kuamua kufunguka rasmi.

“Nas ni kijana mpole sana na wala hana tatizo, wote tumekuwa tukitoka mji mmoja wa Queens jijini New York, hivyo yeye ni kama Mfalme wa Hip Hop kwenye mji wa Queens na mimi ni kama Queen wao.

“Sina tatizo lolote na Nas na kila kitu kipo sawa, siku za hivi karibuni nilishinda nyumbani kwake na nililala huko, hivyo naweza kusema kila kitu kipo vizuri kwa sasa.

“Niliwahi kusema kuwa sina mpango wa kuwa na mwanaume kwa sasa kwa kuwa nawachukia, lakini kutokana na jinsi nilivyo na Nas, chochote kinaweza kutokea,” alisema Nicki.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here