25.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 20, 2023

Contact us: [email protected]

Mimi Mars hataki kuchanganya muziki na mapenzi

Na GLORY MLAY

MSANII wa Bongo Fleva, Marianne Mdee maarufu kwa jina la Mimi Mars, amesema hataki kuchanganya uhusiano na kazi za muziki.

Mimi Mars ambaye ni mdogo wake Vanessa Mdee, alisema kwa sasa hayupo kwenye uhusiano, lakini pindi akiingia hapendi kuyaweka wazi kukwepa watu kuchanganya na kazi zake.

“Kiukweli sipendi kuuanika uhusiano wangu, masuala ya mapenzi sitaki kuyazungumzia kabisa kwa sababu sitaki iwe kipaumbele changu, nina kazi nyingi za kufanya hivyo sio vizuri kuchanganya na uhusiano wangu kwa kuwa watu nawajua,” alisema mrembo huyo.

Hata hivyo aliongeza kwa kusema, akili yake kwa sasa ipo kwenye muziki kwa kuwa ana lengo la kufika mbali, hivyo masuala ya uhusiano yatakuja baadae.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
210,784FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles