NYOTA wa muziki nchini Marekani, Teyana Taylor, amevishwa pete ya uchumba na staa wa mchezo wa kikapu ambaye anakipiga katika timu ya Cleveland Cavaliers, Iman Shumpert.
Hatua ya kuvishwa pete kwa Teyana imetokea mara baada ya kugundulika kwamba msanii huyo ana ujamzito wa staa huyo wa kikapu nchini Marekani.
Wawili hao wanatarajia kupata watoto pacha, hivyo kupitia mtandao wa Instagram, Teyana ameweka picha wakiwa wawili na mpenzi huyo na kusema kuwa kila kitu kipo mbioni baada ya kuvishana pete.
“Asante sana Shumpert kwa kuyabadilisha maisha yangu, naweza kusema kuwa wewe ni mume wangu, nakukaribisha katika familia yangu, ninaamini tutakuwa wote milele,” alisema Teyana.