30.2 C
Dar es Salaam
Sunday, March 26, 2023

Contact us: [email protected]

Milioni 750/- zagharamia mkutamo ALAT

NA MWANDISHI WETU-MWANZA

BENKI ya NMB imesaidia zaidi ya Sh milioni 750 kwa mikutano mikuu ya Jumuiya ya Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa (ALAT) kwa miaka mitano mfululizo, huku ikiahidi kuendelea kushirikiana na Serikali za mitaa nchini kutatua changamotoi mbalimbali.

Hayo yalisemwa juzi jijini hapa na Ofisa Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati wa NMB, Filbert Mponzi wakati akikabidhi udhamini wa benki hiyo kama mdhamini mkuu wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa ALAT unaoanza leo Hoteli ya Malaika Beach.

Mponzi alisema benki hiyo inatambua mahusiano ya kibiashara yaliyopo kati yake na ALAT kupitia zaidi ya halmashauri 180 ambazo inashirikiana kukusanya mapato ya Serikali huku akisema kusema kuwa taasisi hiyo ni mbia wa karibu na Serikali, hivyo mahusiano yao na jumuiya hiyo yameanza muda mrefu uliopita.

 “Tumepeleka huduma zetu nchi nzima huku tukizifikia zaidi ya halmashauri 180 tukiwahudumia katika nyanja mbalimbali za kibenki kuanzia wafanyakazi, wafanyabiashara na wajasiriamari  na pia madiwani, na hii inaonyesha utayari wetu wa kuhudumia Serikali za Mitaa,” alisema Mponzi.

Mwenyekiti wa ALAT Taifa, Gulamhafeez Mukadam, aliishukuru NMB kwa kuonesha kujali Serikali za mitaa na mchango wa mwaka huu unaonesha dhamira na ushirikiano wa kweli kati ya taasisi hizo mbili.

Alisema kuwa Serikali za mitaa na mamlaka zake bado zinakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinahitaji kushikwa mkono na taasisi kama NMB kusaidiana kutatua changamoto hizo.

Aliiomba pia NMB kuangalia namna ya kuangalia upya misaada yake inayotolewa kwa jamii kupitia uwajibikaji kwa jamii (CSR), akiiomba kuanza kusaidia jambo ambalo mwisho linakuwa kubwa kuliko misaada midogo midogo ambayo inaweza ikawa na mchango mdogo kwenye jamii.

Mjumbe wa Kamati  ya Utendaji ya ALAT  ambaye pia ni Meya wa Manispaa ya Sumbawanga, Justine Malisawa aliishukuru NMB kwa kuleta mfumo wa ukusanyaji mapato ya halmashauri kielektroniki na kuisifia kuwa imeleta mafanikio makubwa kwa mapato ya Serikali kuongezeka tofauti na ilivyokuwa zamani hasa ndani ya miaka hii mitatu.

Kauli hiyo iliungwa mkono na Mbunge wa Viti Maalumu  Mkoa wa Pwani ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya ALAT, Zaynab Vulu, ambaye alisema benki hiyo imejipambanua kwa kufika maeneo ambayo benki nyingine hazijafika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,195FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles