28.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Milioni 584 zawezesha Kata kujenga shule Sekondari

Na Malima Lubasha, Serengeti

SERIKALI imetoa Sh milioni 584 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya sekondari katika Kata ya Nagusi Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti mkoani Mara, ili kuwaondolea usumbufu watoto wanaotoka kata hiyo kwenda kata nyingine kufuata elimu.

Diwani wa Kata ya Nagusi Tarafa ya Grumeti, Andrew Mapinduzi amesema hayo wakati akizungumza na Mtanzania Digital kuhusu maendeleo ya sekta ya elimu katika kata hiyo ambayo haikuwa na shule ya sekondari ambayo imejengwa eneo lenye kubwa wa hekta 15.

Diwani Mapinduzi alisema kata hiyo haikuwa na shule ya sekondari hivyo wanafunzi wanaomaliza darasa la saba na kuchaguliwa kujiunga na sekondari walilazimika kwenda shule za kata jirani za sekondari  ya Rigicha pamoja na Nagusi iliyopo umbali zaidi ya kilometa 6.

Alisema utaratibu wa shule hiyo kusajiliwa unaendelea kuchukuwa wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa mwaka wa masomo 2024 na watoto wanaotarajiwa kujiunga kutoka shule za msingi kata hiyo waliofaulu ni 147.

Alisema kuwa katika ujenzi huo wananchi wa kata hiyo wamechangia asilimia 20 ya gharama ya fedha zilizotolewa na serikali kwa kutoa tripu 68 zamawe,tripu 42 za mchanga,kokoto tripu 2 pamoja na kufa nya usafi wa eneo kama nguvu kazi  kiasi cha Sh milioni 8.88.

Diwani Mapinduzi alifafanua kuwa wamekamilisha ujenzi wa jengo la utawala, madarasa nane, vyoo matundu nane, maabara tatu za fizikia, kemia na baiolojia, maktaba moja na Tehama moja pamoja na madawati 320 kwa madarasa yote ambapo hivi sasa wanakamilisha kwa kuweka vigae na kupaka rangi.

“Walimu wanne akiwemo mwalimu mmoja wa kike wamepangwa katika shule hiyo inayotajiwa kupewa jina la Chief Sarota Sekondari School,” alisema Mapinduzi.

Alisema ujenzi wa nyumba kwa ajili ya walimu unatarajiwa kuanza awamu ya pili baada ya ujenzi huu awa mu ya kwanza kukamilika.

Aidha kwa vile wananchi wa kata hiyo wengi ni jamii ya wafugaji shule imejengwa umbali wa kilometa 5 kutoka mpakani mwa hifadhi ya Serengeti wanakusudia kujenga bweni  amba po ameipongeza serikali kutoa fedha hizo za ujenzi wa sekondari hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles