28.3 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Milioni 130/- zajenga studio ya muziki Sinza

Ally HapiNA MWANDISHI WETU

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi, amezindua studio ya kisasa ya Kaburu Record iliyogharimu Sh milioni 130.

Mmiliki wa studio hiyo iliyopo Sinza Palestina ametakiwa na mkuu huyo wa wilaya kuhakikisha anakuza vipaji vya wasanii wachanga ili wafikie mafanikio.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika juzi, Hapi alisema Serikali inaunga mkono uwekezaji uliofanywa na vijana hao na kwamba ni wakati sasa wa wenye vipaji kupata ajira kupitia vipaji vyao ili wajikwamue kimaisha,” alisema.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa studio hiyo, Msafiri Peter ‘Papa Misifa’, alisema:

“Najivunia kufanyakazi na wasanii wenye majina makubwa kwa sasa katika muziki nchini akiwemo Diamond, Rich Mavoko, Timbulo, Dayna na wengine hivyo tutaiendesha ili kutimiza malengo na mafanikio ya wasanii wanaochipukia,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles