Miley Cyrus amlilia Nguruwe

0
771

MIAMI, MAREKANI

STAA wa filamu na muziki nchini Marekani, Miley Cyrus, ameshindwa kuzuia hisia zake baada ya Nguruwe wake ambaye anajulikana kw ajina la Pet Pig Pig.

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 26, ametumia ukurasa wake wa Instagram kumlilia Nguruwe huyo huku akiwaambia mashabiki atakuwa na kipindi kigumu kwa siku za hivi karibuni.

“Nilikuwa na kipindi kigumu na kizuri tangu mwaka 2014 nilipokuwa na Pet Pig Pig, nitavikumbuka vipindi hivyo vyote kwa kuwa nilimzoea sana, lakini sasa sitomuona tena kwenye maisha yangu,” aliandika mrembo huyo.

Mbali na kuandika maneno hayo, lakini msanii huyo alitumia ukurasa huo kuposti picha mbalimbali za kumbukumbu akiwa na Nguruwe huyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here