26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

‘Mikusanyiko huweza kusababisha matatizo ya moyo kwa watoto’

Aveline Kitomary -Dar es salaam

DAKTARI bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Sulende Kubhoja, amesema kuwa mikusanyiko huweza kusababisha magonjwa ya moyo kwa watoto.

Dk. Kubhoja pia alisema kuwa endapo mtoto atazaliwa katika kituo cha afya,  ataweza kuepuka kupata magonjwa ya moyo kutokana na kupata uangalizi na vipimo.

Akizungumza na MTANZANIA katika mahojiano maalum, Dk. Kubhoja alisema ni vyema sasa wazazi wakazingatia maelekezo yanayotolewa na wahudumu wa afya ili kuepuka matatizo ya moyo kwa watoto.

“JKCI tunapokea wagonjwa nchi nzima, hata nje ya nchi, kwa wastani wa siku tunaona wagonjwa 30 kwa upande wa watoto. Kila siku tunafanya operasheni kwa watoto wawili kwa sababu zinachukua muda na gharama nyingi na  katika wagonjwa 30 wanaokuja wengi wana hitilafu ya moyo ya kuzaliwa nayo na wanaobaki ni kutokana na magonjwa ya kuambukizwa.

“Kinga ni bora kuliko tiba, kuna vitu  ambavyo tafiti zilishafanyika, kwamba  kinga kwa kutumia chanjo inasaidia, hivyo tunahimiza watu kuchangamkia chanjo, kingine ni kuwakinga watoto na maambukizi, wanaweza kupata chanjo, lakini ni vizuri kuwazuia watoto wasiambukizwe,” alifafanua Dk. Kubhoja.

Alisema kwa sasa kumekuwa na wimbi kubwa la watoto kupelekwa shule za awali wakiwa kwenye umri mdogo, huku kukiwa na msongamano katika shule zao, hali ambayo ni hatari kwa afya ya moyo.

“Utakuta mtoto ana miaka miwili au  mitatu bado hajajua kujitegemea, kujituza, kujisafisha na kule darasani wanakusanywa kwa pamoja, utakuta hapo mwingine anakohoa, mwingine kupiga chafya, wanaambukizana magonjwa ya njia ya hewa.

“Kwahiyo ni vizuri  mtoto akianza shule kinga yake ya mwili iwe imara  hivyo mikusanyiko haifai kwa watoto, tuwaepushe watoto na mikusanyiko mingi isiyokuwa na sababu na ndo maana haturuhusu watoto kutembelea wagonjwa hospitali kwa sababu wanaweza kuambukizwa magonjwa mengine,” alisisitiza Dk. Kubhoja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles