29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Mikopo ya ‘kausha damu’ bado mwiba-Serikali

*…yatoka mikopoa ya Trilioni 5.6 kwa Watanzania

Na Ramadhan Hassan,Mtanzania Digital

Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi(NEEC) limekiri bado kuna changamoto ya Watanzania kukopa mikopo kausha damu bila kujua fedha hizo wanaenda kuzifanyia nini.

Kutokana na hali hiyo limeshauri wanaokopa kujua wanatakiwa kufanya biashara gani na marejesho yake yatakuwaje.

Hayo yameelezwa Februari 14,2023 na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Being’i Issa wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu majukumu ya Baraza hilo kwa kipindi cha mwaka 2022/2023.

Katibu Mtendaji huyo amesema bado kuna changamoto ya watanzania kukopa na kwenda kulipa ada ama kufanya matumizi mengine.

“Tusikimbilie kukopa wakati hujui utafanyia nini wengi wanaenda kwenye ile mikopo kausha damu, unakopa asubuhi unaanza kulipa jioni ama kesho yake,matokeo yake anakuja kusombewa makochi na vitanda,”amesema Katibu Mtendaji huyo.

Hata hivyo, amesema Baraza hilo limekuwa likitoa elimu jinsi ya kukopa kupitia mifuko mbalimbali.

“Tatizo ni kubwa na sasa tunakazania elimu ya mikopo ianze kufundishwa kuanzia ngazi ya shule za sekondari ili wanafunzi wajue mapema,mtu ana milioni moja amekopa anapeleka katika ada, sasa unajiuliza mkopo atalipaje?,”alihoji Mtendaji huyo.

Beng’i amesema kumekuwa na jitihada za kuwasaidia wajasiriamali kwenye suala la vifungashio vyenye ubora.

Amesema wanajikita kuwafikia zaidi wanawake wajasiriamali kwa kuhakikisha wanafanikiwa katika biashara zao.

Amesema mwaka 2022 Serikali imetoa mikopo kwa Watanzania milioni 9.8 yenye thamani ya Sh trilioni 5.6 kwa ajili ya kuwawezesha wananchi kiuchumi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles