27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

MIKOPO PSPF YAZIDI KUWANUFAISHA WANACHAMA WAKE

NA HARRIETH MANDARI–DAR ES SALAAM


WATANZANIA wanachama katika mifuko ya pensheni nchini, wamekuwa wakinufaika na huduma mbalimbali za mifuko hiyo zinazowawezesha kutoa suluhu ya changamoto mbalimbali za kimaisha zikiwemo huduma za afya na mikopo mbalimbali.

Moja ya mifuko ambayo wanachama wamenufaika na huduma za mikopo ni wanachama wa Mfuko wa PSPF ambapo kwa mujibu wa Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Abdul  Njaidi, ni muhimu kwa wanachama wa mifuko ya pensheni nchini kupitishia mikopo ya wanachama wake kwenye mabenki.

Anasema wanachama wa PSPF  hupatiwa huduma ya mikopo mbalimbali kupitia benki za CRDB na benki ya Posta (TPB).

“Mfuko huu unashirkiana na benki za Posta na CRDB kwa sababu  inakuwa rahisi zaidi kwa wanufaika kupatiwa mikopo kwa haraka zaidi,” alisema.

Akifafanua  kuhusu umuhimu wa utoaji mikopo hiyo kupitia benki, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya   Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii ( SSRA), Sarah Kibonde, anasema kwa mujibu wa sheria ni lazima huduma ya mkopo kupitishiwa katika mabenki badala ya kumpatia mteja moja kwa moja.

“Mojawapo ya majukumu ya mifuko hiyo ni kuhamasisha wateja kujiunga na mfuko huo, kukusanya michango na pia uwekezaji, hivyo inapotokea wanaanzisha huduma hizo za mikopo kama sehemu ya kuwajali na kuwezesha wateja wao, ni lazima wahakikishe wanashirikiana na benki kwa kupitishia mikopo hiyo katika na  kinyume na hilo watakuwa wamekwenda kinyume na majukumu yao husika,” anasema.

Mfuko wa Pensheni wa PSPF una aina mbalimbali za mikopo ambapo kundi la kwanza linalonufaika na huduma hiyo ni la wanachama wachangiaji.

Kwa mujibu wa Njaidi, ili kuongeza wigo wa huduma na fursa kwa wanachama wa PSPF, mfuko uliingia makubaliano na benki za TPB na CRDB ili kuwawezesha wanachama wake kupata huduma za mikopo ya muda mfupi kupitia benki hizo.

Alisema ushirikiano huo kati ya mabenki na mfuko huo unawezesha wanachama kupata huduma kwa ukaribu zaidi na maeneo yao ya kazi. Mikopo hiyo imegawanyika katika makundi mawili ambapo kundi la kwanza ni la wanufaika wa mkopo ambao ni wanachama wachangiaji na mikopo ya kundi hilo ipo katika makundi mbalimbali yakiwemo; mkopo wa kuanza maisha (Jipange kimaisha na PSPF) unaolenga kumpunguzia mwanachama mpya changamoto zitokanazo na kumudu gharama za maisha ya ajira ambapo mwanachama anayenufaika ni yule aliyechangia mfuko kwa miezi kati ya sita na kipindi kisichozidi miezi 12.

Pia kuna mkopo wa elimu; hii ni kwa wanachama waliochangia mfuko kwa miezi 24 ambapo kwa ngazi yoyote ya elimu aliyonayo, mwanachama anakopeshwa ada inayolipwa moja kwa moja na mfuko katika chuo anachosoma.

Aidha katika kundi hili kuna mkopo wa viwanja vya makazi (Nipo site na PSPF); mkopo huu ni kwa mwanachama yeyote aliyechangia mfuko huo kwa miezi sita na marejesho ya mkopo huo ni kwa miaka mitatu hadi mitano.

Kundi la pili la wanufaika ni mkopo kwa wastaafu wa mfuko huo.

Kwa upande wa mifuko mingine ikiwemo Mfuko wa Pensheni wa LAPF, pia hutoa huduma mbalimbali za mikopo ikiwemo mkopo wa nyumba na huduma ya mkopo kwa wanachama kupitia Saccos.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles