27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Mikoa mitatu yashika mkia chanjo za watoto

MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

MIKOA ya Katavi, Shinyanga na Tabora, imetajwa kuwa ya mwisho katika utoaji chanjo za kinga kwa watoto jambo ambalo ni hatari kwa afya na jamii kwa ujumla.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa Health Promotion Tanzania (HDT), Dk. Peter Bujari, alisema ipo haja kwa Serikali kuangalia hali hiyo ili kujenga taifa lenye watu wasiokuwa na maradhi.

Alisema licha ya suala la afya kwa wote kuwa moja ya ajenda, lakini bado kwa mikoa hiyo inatakiwa iangaliwe kwa umakini na kujua tatizo la kina kwanini chanjo kwa watoto hazikumalizika kama inavyotakiwa.

“Chanjo kwa mtoto zipo karibu tisa, lakini na kila chanjo ina umuhimu wake, nasi HDT tuliangalia masuala kadhaa ikiwamo suala la umbali wa vituo vya afya, lakini pia uwepo wa mila potofu ni moja ya kikwazo kwa hali hii.

“Kwa mfano ukiangalia takwimu za Serikali za hali ya afya nchini za mwaka 2016 hali bado si nzuri. Katavi ina asilimia 54, Shinyanga asilimia 56 na Tabora asilimia 59, sasa hapa unaona bado hali si nzuri.

“Lakini pia hata ukiangalia vizuri maeneo ambayo hasa watoto wanatimiza chanjo muhimu ni mijini kuliko vijijini.

“Kwani hata pindi inapoweza kutokea mlipuko wa maradhi hali itakuwa mbaya zaidi na maana yake ni kwamba watoto 113,000 hawajafikiwa na chanjo ikiwamo kumaliza kabisa. Kwa hiyo kati ya watoto 46 kwa 100, hawajapata chanjo katika mikoa ya Katavi, Shinyanga na Tabora,” alisema Dk. Bujari.

Alisema Serikali inatakiwa kuwa na mpango madhubuti kwa ajili ya kutoa chanjo kwani jamii ipo hatarini kupata maradhi.

“HDT tunawaomba wabunge sasa wasimamie Serikali ihakikishe inatoa chanjo sambamba na ujenzi wa vituo vya afya.

“Pia tunatambua kazi kubwa iliyofanywa na Serikali maana miaka ya nyuma tulikuwa tukiona maradhi kama pepo punda, surua na polio ambayo kwa sasa hayapo tena,” alisema Dk. Bujari.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles