26.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, March 26, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Mikoa 16 kunufaika na Nishati ya Jotoardhi

Na Mwandishi Wetu

Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Felchesmi Mramba, amesema mikoa 16 nchini itanufaika na maendeleo ya nishati ya Jotoardhi na kuifanya kuwa msingi wa mkakati wa nishati endelevu.

Ameyasema hayo katika mjadala wa viongozi wanaoshiriki mkutano wa Kimataifa wa Nishati Endelevu kwa wote (SEforALL) unaofanyika katika jiji la Bridgetown nchini Barbados.

Mramba amesema nia hiyo inajidhihirisha kupitia uanzishwaji wa Kampuni ya Maendeleo ya Jotoardhi Tanzania (TGDC) kwa lengo la kutafiti na kuendeleza rasilimali za Jotoardhi ambapo hadi sasa kampuni hiyo inafanya kazi katika maeneo zaidi ya 50.

Ameeleza kuwa Tanzania imelenga kuunganisha nishati hiyo kwenye Gridi ya Taifa ifikapo mwaka 2030 ili kuwa na umeme wa uhakika unaotokana na nishati jadidifu kuelekea Dira ya Tanzania 2025 ambayo inasisitiza maendeleo endelevu ya nishati kama nguzo ya mabadiliko ya kiuchumi.

“Lengo letu ni kuunganisha nishati ya Jotoardhi kwenye gridi ya taifa ifikapo 2030, suala hili ni miongoni mwa azma yetu pana ya kuhakikisha upatikanaji wa umeme kwa wote ifikapo 2030 ili kuondokana na uzalishaji wa hewa ukaa ifikapo 2050.

“Hii ni kutokana na Sera ya Taifa ya Nishati ya Tanzania 2015 yenye mpango mkuu wa Nishati 2020 pamoja na tamko la Dar es Salaam la “Mission 300” katika mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika wa 2025,”. amesema Mramba.

Aidha amesema ili kuvutia uwekezaji, Serikali imeweka mfumo madhubuti wa sera na udhibiti kuvutia wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali ili kufanya tafiti na kufungua uwezo kamili wa rasilimali hiyo kuwa chachu kwa taifa.

“Kwa kutambua umuhimu wa kimkakati, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeipa kipaumbele nishati ya Jotoardhi katika ajenda ya kitaifa ya maendeleo ya nishati,” amesema.

Naye, Waziri wa Nishati wa Shirikisho la St. Kitts na Nevis, Konris Maynard amesema nchi zinatakiwa ziwe tayari kukuza matumizi ya Jotoardhi na kuhama katika matumizi ya nishati zisizo salama kwa mazingira na kuwataka wadau walioshiriki mkutano huo kuendelea kuhamasisha matumizi ya nishati hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
596,000SubscribersSubscribe

Latest Articles