Mijusi ya ajabu usiyowahi kukutana nayo

0
951

Mwandishi Wetu

JAMII mpya ya mijusi imetambuliwa miaka ya hivi karibuni. Mmoja kati ya mijusi hiyo ni yule mwenye tabia ya kujivua magamba yake mwilini na kumuacha adui anayetaka kumla, pindi anaposhambuliwa.

Jamii nyingi za mijusi hukata mkia, wanaposhambuliwa, lakini huyu aliye na magamba kama samaki, ana magamba mengi mno yanayotoka kwa urahisi.

Mjusi huyu aliyetambuliwa, wanasayansi wanasema ni bingwa wa usanii, wakiwa na kiwango kikubwa mno cha magamba kuliko aina yoyote ya mjusi duniani.

Ngozi yake inayofanana na magamba ya samaki, ina mtindo wa kukatika katika.

Sehemu kubwa ya magamba hayo yameshikanishwa na eneo dogo mno mwilini na kuwa rahisi kubabuka.

Aidha, ndani ya magamba hayo kwenye ngozi, kuna maeneo ya kukatika katika.

Hata ingawa jamii nyingi ya mijusi, hawawezi kupoteza ngozi zao kwa urahisi hadi pale wanapokabwa kwa nguvu, mjusi huyu ana uwezo huo haraka anapoguswa.

Ajabu ni kwamba, ngozi na magamba mengine humea kwa kasi ya ajabu, kwa kipindi cha wiki chache tu.

Jamii hiyo ya mujusi imegunduliwa katika maeneo ya mapango ya Tsingy, Kaskazini mwa Madagascar.

MJUSI MKUBWA DUNIANI

Huyu ni aina nyingine ya mjusi ambaye anatajwa kuwa mkubwa kuliko wote duniani.

Amphibia huyo mwenye mwonekano wa mjusi ana upana wa mita mbili na anapatikana Kusini mwa China.

Mjusi huyo mkubwa amekuwa ni miongoni mwa wanyama wa porini wanaoogopwa zaidi.

Wanasayansi wanasema kwamba watu wa hifadhi ya wanyama wanapaswa kufanya jitihada za kumuokoa mjusi huyo ama la anaweza kupotea.

Mwanzoni, mjusi huyo mkubwa alidhani kuwa ndiye peke yake ambaye ana ukubwa kiasi hicho.

Lakini utafiti unaonyesha kuwa wapo amphibia watatu wa aina hiyo katika maeneo mbalimbali nchini China.

Ingawa amphibia aliyepatikana Kusini mwa China , ndio mjusi mkubwa zaidi kati ya hao watatu.

Hata hivyo, watafiti wanadhani kuwa huyo ndio amphibia pekee mkubwa ambaye yuko hai.

Profesa Samuel Turvey kutoka Jumuiya ya Wataalamu wa Zoolojia mjini London, anasema kuwa idadi ya wanyama pori imeongezeka kwa kasi.

“Tuna imani kuwa kutakuwa na ueleo mpya wa kuhifadhi wanyama na hatua za haraka zinapaswa kuchukuliwa ili kulinda uwapo wa viumbe hai hao,” anasema mtafiti.

“Utafiti huu unakuja wakati ambao China inapaswa kuwalinda amphibia wakubwa walioko porini,” anasema Melissa Marr, mtafiti wa masuala ya kihistoria.

Mijusi mikubwa ilionekana katikati ya nchi hiyo, mashariki na kusini mwa China.

Miaka ya hivi karibuni, soko la vyakula vya starehe limeongezeka nchini humo hivyo kufanya idadi ya uwindaji wa wanyama pori kuongezeka pia.

Wanasayansi walitumia viumbe hai ambavyo vina mwonekano sawa na mjusi mkubwa anayepatikana China na kuangalia asili ya mnyama huyo ni wapi.

Wazo lilikuwa ni kuona kama mjusi wa China ana tofauti na mjusi mkubwa aliyedaiwa kuwa mkubwa mwaka 1920 ambaye amehifadhiwa nchini Uingereza.

Walitaka kujua kama ana tabia sawa na mjusi huyo mpya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here