25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

MIJI 10 BORA KWA WANAFUNZI WA KIMATAIFA 2017

Mwonekano wa mji wa Vancouver nchini Canada

 

 

NA JOSEPH LINO,

VYUO vikuu vingi vya kimataifa vimejenga katika miji maarufu katika nchi mbalimbali duniani, chuo kuwa katika mji fulani kunatoa fursa muhimu kwa wanafunzi wa taaluma husika. 

Kila mji unafursa kadhaa za kitaaluma na maisha ya kawaida ya kila siku. 

Wataalamu wa vyuo vikuu wametoa ripoti ya miji yenye wanafunzi bora katika mwaka huu.

Ripoti hiyo imetolewa kutokana na unafuu wa maisha na uzoefu wa wanafunzi, fursa za kazi kwa vitendo na mazingira rafiki kwa wanafunzi wa kimataifa.

Mji wa Vancouver, Canada 
Mji wa Vancouver ni miongoni mwa miji yenye mazingira mazuri ya asili kusoma, asilimia 44 ya wanafunzi wanaosoma katika vyuo vya mji huo hubakia kwenye mji baada ya kuhitimu masomo yao. Mji huo unafursa kadhaa hasa kwa wanafunzi wa kimataifa.

Munich, Ujerumani
Munich ni mji mwingine ambao ni nafuu kusoma, kama inavyojulikana kwamba vyuo vikuu katika mji huo havitozwi ada ya masomo na kwa Ujerumani kwa ujumla, hata hivyo, taasisi ya German Institute for Education and Social Economic Research inatabiri kuwa Serikali ya Ujeremani itarudisha ada katika vyuo vikuu nchini humo.

Boston, Marekani
Mji wa Bostoni nchini Marekani unaheshimika na maarufu kwa wanafunzi wa kimataifa kuwa bora, hata hivyo, gharama za uendeshaji wa maisha ya kila siku ni kubwa mno na vyuo katika mji huo hutozwa ada kubwa. Lakini wanafunzi wa kimataifa wanafursa mbalimbali za kiutaaluma na kazi baada ya kuhitimu masomo.

Toyko, Japan
Mji wa Toyko, Japan katika Bara la Asia, unakadiriwa kuwa na idadi ya watu zaidi ya milioni 38 na maisha ya kila siku ni ghali kwa wanafunzi wa kimataifa ukilinganisha na baadhi ya nchi kama Hong Kong na Singapore barani humo.
Lakini katika uzoefu wa kitaaluma, mji huo unatoa fursa mbalimbali za kuweza kuishi na kwa upande wa gharama ya  vyakula ni nafuu hasa kwa wanafunzi.

Berlin, Ujerumani
Vijana wengi kutoka mataifa mbalimbali duniani kote wanakimbilia katika mji wa Berlin lakini wengi si wanafunzi, asilimia 16 ya wanafunzi wa vyuo vikuu vya Berlin wanatokea mataifa mengine.
Elimu bure katika ngazi ya vyuo vikuu nchini Ujerumani kwa sasa inaufanya mji huo kuwa wenye maisha nafuu kwa wanafunzi wa kimataifa.

Melbourne, Australia
Kwa  upande wa mji wa Melbourne, vyuo vingi hutozwa gharama kubwa ya ada na hufanya maisha ya kila siku kuwa ghali hasa kwa wanafunzi wa kimataifa.
Vyuo vikuu vingi nchini humo na kwa Australia kwa ujumla huwa na ada kubwa ya masomo. 
Hata hivyo, mji huo unamazingira mazuri ya kitaalamu, pia hutoa fursa ya kupata uzoefu wa maisha ya kila siku kwa wanafunzi wa kimataifa
 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles