29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Miili ya waliofarikia ajali ya Kibiti kupimwa DNA

Mwandishi wetu

Ndugu wa karibu wa watu waliofariki kwenye  ajali ya gari iliyotokea wilayani Kibiti mkoani Pwani wametakiwa kujitokeza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), kesho Jumatatu Septemba 2, kwaajili ya zoezi la kufanya uchunguzi wa kulinganisha Vinasaba (DNA) ili waweze kupewa miili hiyo.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma MNH, Aminiel Aligaesha leo Jumapili Septemba 1, ambapo asema zoezi hilo litaanza saa mbili asubuhi na wanaotakiwa kufika ndi ndugu wa karibu hususan baba, mama au mtoto.

“Jana saa tano asubuhi tumepokea miili ya marehemu watano wa ajali ya gari iliyotokea huko Kibiti ambapo imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti hivyo tunawaomba ndugu wa karibu wa marehemu waje kesho saa mbili asubuhi ili kuchukuliwa sampuli na Mkemia Mkuu wa Serikali ili kusaidia kufanya uchunguzi wa kulinganisha vinasaba kati ya ndugu na marehemu  ili waweze kupewa miili hiyo kwa ajili ya mazishi baada ya uchunguzi kukamilika,” amesema.

Aligaesha amesema miili hiyo ambayo ni ya watu wazima wanne na mtoto mmoja imeungua sana hali iliyopelekea utambuzi wao kuwa mgumu lakini tayari wameshafanya uchunguzi na kuchukua sampuli kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi pamoja na Mkemia Mkuu wa Serikali ili kufanya uchunguzi zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles