31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

MIHAN GESI YASHINDA TUZO YA UBORA

Na MWANDISHI WETU-DODOMA


KAMPUNI ya Gesi ya Mihan imetunukiwa tuzo ya Kampuni iliyofanya vizuri kwa mwaka 2016 katika sekta ya usambazaji wa gesi nchini.

Tuzo hizo ambazo ziliambatana na uzinduzi wa ripoti ya  utendaji wa sekta ndogo ya mafuta  kwa mwaka 2016 ambapo  zilitolewa mwishoni mwa wiki mkoani hapa.

Tuzo hizo zilitolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati, Maji na Mafuta (EWURA).

Akizungumza wakati wa utoaji wa tuzo hizo Mwenyekiti wa Bodi ya Ewura, Profesa Jamidu Kitima alisema sababu za Kampuni ya Gesi ya Mihan kupata tuzo hiyo ni kutokana na kusambaza huduma hiyo katika maeneo mengi ikiwemo vijijini.

Alisema Mihan Gesi wamekuwa wakipatikana kila eneo kuanzia mijini mpaka vijijini hivyo wanastahili kupata tuzo ya kampuni yenye utendaji kazi bora kutokana na kuwafikia watu wengi.

“Mihan Gas wamepata tuzo ya Kampuni yenye utendaji kazi bora katika tasnia ya biashara ya Gesi nchini kwa mwaka 2016 kwani wameweza kufika mpaka vijijini hivyo mgeni rasmi pia utawapatia tuzo,’’alisema

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Ewura, Felix Ngamlagosi alisema katika Sekta ya Mafuta wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya kukosekana kwa viwango mwafaka vya gesi ya kupikia inayotumika nchini.

Ngamlagosi alisema Ewura inaendelea kushirikiana na TBS na wadau wengine ili kuhakikisha nchi inakuwa na viwango vya gesi ya kupikia  (LPG Specifications) vinavyofaa katika mazingira ya nchi yetu.

“Utumiaji mdogo wa LPG nchini unaotokana na kuwa na uwezo mdogo wa miundombinu  ya kuhifadhia LPG,Ewura itaendelea kufanya  uhamasishaji wa matumizi ya LPG na pia kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji katika biashara ya LPG,’’ alisema

Alisema Ewura imeendelea kusimamia biashara ya gesi ya kupikia majumbani (LPG) ili kuhakikisha taratibu husika zinazingatiwa.

Mkurugenzi huyo alisema pia imeendelea kufanya ukaguzi ili kubaini ubora wa mafuta yanayouzwa nchini ambapo katika kipindi cha kuanzia Januari mpaka Desemba 2016, Ewura ilichukua jumla sampuli 354 kutoka kwenye miundombinu mbalimbali ikiwemo vituo vya mafuta, maghala ya kuhifadhia mafuta na magari ya kusafirisha mafuta na kuzipeleka maabara kwa ajili ya kubaini ubora wake.

Alisema kati ya sampuli hizi, sampuli 52 sawa na asilimia 14.6 hazikukudhi viwango vilivyowekwa na Shirika la Viwango la Taifa (TBS).

Pia alisema hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2016, nchi ilikuwa na maghala ya kuhifadhia mafuta (storage depots) yenye ujazo wa lita bilioni 1.2 ambapo  kati ya ujazo huo, lita milioni 999 sawa na asilimia 92 ya ujazo, ni maghala yaliyopo Dar es Salaam.

Alisema kwa ujumla, nchi ina maghala yenye uwezo wa kuhifadhi mafuta yanayotosheleza mahitaji ya nchi kwa zaidi ya siku 120 kwa matumizi ya nchi.

Akizungumzia tuzo hiyo Mkurugenzi wa Mihan Gesi, Hamis Ramadhan, alisema hatua hiyo inatokana na uwekezaji wao walioufanya kwa ajili ya kutoa huduma bora na nzuri kwa Watanzania wote.

“Mihan tumejipanga kutoa huduma bora na gesi yetu ni salama zaidi kutokana na valvu yake ambayo imewekwa na hupatikana kwa bei tofauti. Na mtandao wetu tupo katika kila wilaya ya Tanzania hadi vijijini na ndoto yetu ni kuunga mkono juhudi za Serikali katika utunzaji wa mazingira kwa kumfanya mama na hata mtumiaji mwingine kuwa rafiki wa matumizi ya gesi salama ya kupikia ya Mihan,” alisema Hamis

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles