29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Migogoro 90 inayohusu watoto yatatuliwa Bukoba

Na Renatha Kipaka, Bukoba

Jumla ya migogoro 90 inayohusu Watoto katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera imefanyiwa usuluhishi wa vyombo ya kisheria kwa kipindi cha Januari na Mei, Mwaka huu ili kutoa​ haki kwa​ watoto.

Akizungumza jana Alhamisi Juni 16, 2021 Mwakilishi wa Ofisa Maendeleo ya Wilaya ya Bukoba, Monica Kibetenge wakati wa maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyokuwa na kauli mbinu ya “Tutekeleze ajenda 2040 kwa Afrika inayolinda haki za watoto”, amesema kesi hizo ziligusa maeneo ya utelekezaji wa watoto, mimba za utotoni, ubakaji na ulawiti.

Ameyataja maeneo mengine kuwa ni pamoja na waliozaliwa nje ya ndoa na ukinzani wa sheria.

“Kwa kuchangiana hapa kesi za kutekelezwa watoto zipo 42 mimba za utotoni 21 ubakaji na ulawiti 11 watoto waliozaliwa nje ya ndoa watatu na wakinzani wa sheria wapo 13 kwa kipindi tu cha kuanzia mwezi Januari hadi Mei mwaka huu,”amesema Kibetenge.

Aidha, Kibetenge amesema kwa kujali makuzi na ulinzi wa mtoto wadau wa maendeleo waliweza kuunga mkono juhudi za serikali za kuunda mabaraza ya watoto yenye lengo la kusaidia kupata stahiki.

Amesema mabaraza hayo yamesaidia kupata mafaniko makubwa ya kupunguza matukio yaliyokuwa yana kabiliana na mtoto ya ukatili majumbani na wazazi kuwajibika katika malezi

Mratibu wa asasi ya utetezi wa mama na mtoto (TUODEA) wilaya ya Bukoba, Zainabu Shakiru amesema athari za mtoto huanzia kwenye migogoro ya familia na kusababisha ukoseafu wa uangalizi unastahili kupatiwa mtoto

Amesema watoto kati ya umri wa miaka miwili hadi 17, hukumbana na matatizo ya malezi ya wazazi wao pindi wanapoingia katika mifarakano ya ndoa.

“Unakuta mama ametelekezewa watoto yupo nyumba ya kupanga hana mahitaji baba amekimbia ukimfuatilia na kufungua kesi anaona bora atoe hongo ya kuondoa kesi kuliko kuhudumia familia yake,”amesema Shakiru.

Ameongeza kuwa, tatizo kubwa lipo ngazi ya vijiji ambapo mtoto hawezi kupata msaada wa sheria na utetezi matokeo yake ni kuongeza wimbi la ongezeko kutokupata haki.

Upande wake, Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Bukoba, Privatus Mwoleka, amesema ni muda wa wazazi na wazele kubadilika na kusimamia ulinzi na makuzi bora ya mtoto.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles