22.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 20, 2022

Migne kocha mpya Equatorial Guinea

MALABO, EQUATORIAL GUINEA

CHAMA cha soka nchini Equatorial Guinea, imemtangaza aliyekuwa kocha wa timu ya taifa Kenya, Sebastien Migne kuwa kocha wao mpya.

Migne alifungashiwa virago Agosti mwaka huu huko nchini Kenya baada ya taifa hilo kushindwa kufuzu michuano ya CHAN, kwa wachezaji wanaocheza ligi ya ndani.

Kenya ilishindwa kufanya vizuri kwenye michuano hiyo hatua ya awali baada ya kuchezea kichapo kutoka kwa timu ya taifa Tanzania, Taifa Stars.

Mbali na kuondolewa mapema kwenye michuano hiyo, kocha huyo alianza kunyooshewa kidole kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), huko nchini Misri mwaka huu ambapo mashabiki wa taifa hilo walimjia juu kocha huyo kwa madai timu haikuwa kwenye kiwango kizuri.

Kwenye michuano ya Mataifa ya Afrika, Kenya ilifanikiwa kushinda mchezo mmoja dhidi ya Tanzania, huku ikipoteza dhidi ya Senegal na Algeria.

“Mipango mipya, nchi mpya, changamoto mpya. Nathibitisha kuwa kwa sasa mimi ni kocha mpya wa timu ya taifa Equatorial Guinea,” aliandika kocha huyo kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Rais wa shirikisho la soka nchini Kenya, Nick Mwendwa, ameweka wazi kuwa, kocha huyo alikuwa na mkataba na timu hiyo hadi 2020 na makubaliano hayo yalikuwa wazi kuwa, endapo ataondoka kabla ya kumaliza mkataba wake basi hatolipwa fedha zake.

“Makubaliano yetu yalikuwa ni kumpa mshahara hadi Machi 2020, huku akiwa kwenye nyumba ambayo amepangiwa, gari maalumu iliopo chini ya shirikisho, hivyo kutokana na kuamua kuondoka kwake hatutoweza kumlipa fedha zake,” alisema rais wa shirikisho hilo.

Migne atakumbukwa kutokana na kuifanya Kenya iweze kushiriki michuano ya Mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza baada ya kushindwa kufanya hivyo katika miaka 15.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
199,057FollowersFollow
551,000SubscribersSubscribe

Latest Articles