28.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Migahawa inayotembea kuongeza unywaji wa kahawa nchini

Na Nora Damian, Dodoma

Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB) imezindua migahawa inayotembea ili kuongeza unywaji wa kahawa nchini kutoka asilimia saba hadi kufikia asilimia 15.

Migahawa hiyo iliyozinduliwa kwenye Maonesho ya Wakulima maarufu Nanenae yanayofanyika kitaifa jijini Dodoma, utakuwa ukipelekwa kwenye maeneo yote yenye mikusanyiko ya watu na kutoa huduma ya unywaji wa kahawa.

Akizungumza Agosti 2,2024 na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mkuu wa TCB, Primus Kimaryo, amesema migahawa hiyo pia itasaidia kutoa ajira kwa vijana.

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kahawa, Primus Kimaryo, akizungumza na waandishi wa habari kwenye Maonesho ya Wakulima Nanenane, jijini Dodoma.

“Kilimo cha kahawa kinahusu hasa wazee ambao ndio wamiliki wa mashamba ya kahawa, vijana ilikuwa ngumu kidogo mpaka mzazi afariki au apewe shamba. Tuliona tuje na mradi ambao kijana anaweza kunufaika na zao la kahawa, tumebuni mgahawa unaotembea ambapo kijana anaweza akauza kahawa akapata kipato,” amesema Kimaryo.

Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, mgahawa huo ambao utakuwa katika pikipiki ya miguu mitatu (bajaji) na vifaa vya kisasa vya kutengeneza kahawa unagharimu Sh milioni 30 na kijana husika atakopeshwa na kulipa kwa miaka mitatu kisha unakuwa mali yake.

Amesema migahawa hiyo itasambazwa katika maeneo yote yenye mikusanyiko nchini na tayari wana mpango wa kupeleka katika vyuo vikuu mbalimbali nchini.

“Lazima kijana awe anapenda biashara hii na awe anajua kuendesha bajaji, awe anaijua kahawa na aweze kuitengeneza, tayari vijana wengi wameonesha nia ya kutaka kufanya biashara hii,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles