25.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Makala: ‘MICROBIOLOJIA’ uoteshaji vimelea vya magonjwa unavyofanikisha uchunguzi wa dawa na vipukusi-1

Aveline Kitomary

‘Microbilojia’ hii ni Sayansi ya utafiti wa viumbe vidogo kama vile bakteria visivyooneka kwa macho ya kawaida ila kwa kutumia microscope. Viumbe hivi vidogo (micro-organism) vinaweza kuishi sehemu yoyote Ulimwenguni, licha ya kuwa na madhara wakati mwingine lakini pia huwa uwepo wake ni muhimu kulingana na mazingira husika.

Katika maabara mbalimbali hufanyika ‘Micro bio challenge test’ hii humaanisha uwezo wa sampuli kuua vimelea au wadudu waliokusudiwa.

Mchunguzi wa microbiolojia, Msumari Waridi, akionesha vimelea vilivyoota

Mchunguzi wa Microbiolojia kutoka Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA) Kanda ya Ziwa, Waridi Msumari, anasema kwa kutumia maabara ya microbilojia wanaangalia uchafuzi wa vimelea unaoweza kutokea katika bidhaa zote zinavyodhibitiwa na Mamlaka kama dawa, vifaa tiba, vitendanishi na vipukusi.

“Kwenye dawa tunaangalia ‘microbialcontamination’ na kwenye vipukusi tunafanya ‘challenge testing’ ambapo tunaangali uwezo wa kile kipukusi kama detto, Hydrogen peroxide, Iodine, Methylated spirit kuweza kuua kabisa au kupunguza kiwango cha  wadudu ili iweze kutumika kama inavyotarajiwa..

Uchunguzi wa Vipukusi

“Katika uchunguzi wa vipukusi, hatua ya kwanza ni  kuandaa mahitaji yako kama vile ‘culture media’ na reagents utakazozitumia kulingana na njia ya uchunguzi (test method) utakayo itumia,” anasema Waridi.

Aidha, Waridi anasema kwa kila ‘culture media’ kila mtengenezaji ameandika namna ya kuiandaa hivyo maelekezo yanatakiwa kufatwa.

“Hatua ya pili utaenda kwenye usafishaji (Sterilization) ya vifaa na culture media zako ili  kuweza kuua wadudu waliko katika vifaa  na Kuhakikisha ni visafi kwa matumizi ya kichunguzi.

“Baada ya hapo hatua inayo fuata ni kuandaa sampuli yako ya kipukusi unayotaka kuichunguza kwa kufuata maelekezo ya matumizi yaliyoandikwa na matengenezaji kwenye lebo ya sampuli’ kasha unaweka wadudu (reference microorganism) kwa kiasi kinachojulikana na kilichoelekezwa kwenye njia ya uchunguzi (test method) kwa mfano 107 cfu/ml. .

“Baada ya hapo unaacha mchanganyiko huo wa kipukusi na wadudu kwa muda wa dakika 10 ili kuruhusu kipukusi hicho kufanya kazi yake ndani ya muda huo na baada ya hapo unakuja kusimamisha utendajikazi wa kipukusi hicho (neutralization) kwa kuweka kemikali maalum ili uweze kusoma wa kipukusi hicho kufanya kazi yake ndani ya muda unao takiwa,” anasemka Waridi.

Sambamba na hayo, Waridi anafafanua zaidi kuwa; “Unaweka baada ya dakika 10 unakuja kusimamisha utendaji kazi ili uweze kusoma uwezo na  ufanisi wa kile kipukusi ndani ya dakika 10 (antimicrobial activity) kwani inawezekana baada ya pale kipukusi kinaweza kuendelea kufanya kazi sasa ili tujue kuwa ndani ya dakika 10 kipukusi kinafanya kazi unakiondolea uwezo wa kuua wadudu kwani inatakiwa ndani ya dakika hizo tu,”anabainisha Waridi.

Anaeleza kuwa zipo kemikali kama vile, Tween 80 ambayo wanaitumia kuondoa uwezo wa kipukusi ambayo inatakiwa kuua wadudu ndani ya dakika 10.

“Unaichukua tween 80 unaweka ndani ya mchanganyiko wa sampuli yako na wadudu, matarajio ni kwamba ile itaenda kuangamiza uwezo wa kile kipukusi wa kuua wadudu na kama wadudu  watakufa itakuwa ni ndani ya zile dakika 10 za mwanzo na sio baada ya hapo.

“Baada ya hapo unachukua mchanganyiko huo unaweka kwenye sahani maalum za kuoteshea wadudu (petri dishes) na kuweka chakula cha wadudu (culture media) na mwisho kabisa unaweka sahani hizo kwenye kifaa kiitwacho incubator na kuziacha kwa muda maalum unaotajwa kwenye njia ya uchunguzi iliyotumika na baada ya muda huo kama wadudu wapo  wataanza kuota kama hawapo hawataota,” anasema.

Anaongeza “Wapo wadudu wanaoota baada ya saa 24 mpaka 48 kama bacteria, lakini kwa fangas inachukua siku tano baada ya hapo unaanza kusoma majibu na wadudu wameota, utawahesabu na utaenda kufanya hesabu za kujua wadudu wameota kwa asilimia ngapi kulinganisha na kiasi cha wadudu waliowekwa mwanzoni mwa uchunguzi.

“Kisha utalinganisha na mwongozo kama  sampuli yako imefaulu au imefeli. Vilevile kama wadudud hawajaota kabisa maana yake ni kwamba kipukusi hicho kimefanikiwa kuuwa wadudu wote kwa asilimia 100 hivyo kimefaulu,” anasema.

MICROBIOLOJIA YA DAWA

Waridi anasema kwa upande wa dawa kuna aina tofauti tofauti za chunguzi zinazoweza kufanyika kulingana na aina ya dawa.

Itaendelea…

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles