33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mick Schumacher amuinua baba yake kitandani kwa taji

BADI MCHOMOLO NA MITANDAO

NI miaka sita sasa tangu bingwa wa mbio za magari za Formula One, Michael Schumacher, alipopata ajali ya kuanguka kwenye mchezo wa kuteleza kwenye bara­fu na kupoteza fahamu kwa miezi minne.

Desemba 29, mwaka 2013, alipotokea ajali hiyo, iliwashangaza wengi baada ya kutokea kwa taarifa hiyo huko nchini Ufaransa, huku wengi walitarajia kuisikia habari hiyo kwenye mchezo wa mbio za magari na sio mabarafu.

Tangu apate fahamu bado yeye ni mtu wa muda mwingi kuutumia akiwa kitandani kutokana na hali yake kutokaa vizuri kama ilivyo awali. Tatizo kubwa ambalo linamsumbua ni kichwani ambapo aliripotiwa kuumia sana na hata madaktari hawakuwa na uhakika kama angeweza kuwa hai hadi kufikia sasa.

Mbaili na kuugua kwa kipindi kirefu, anapata furaha pale anapoangalia mashindano ya Formula One kwa kupitia runinga, mchezo huo wa mbio za magari ni mmoja kati ya ile ambayo inampa furaha akiwa kitandani.

Mtoto wa Schumacher, ambaye anajulikana kwa jina la Mick Schumacher, aliamua kuingia moja kwa moja kwenye mchezo huo ili kumuenzi baba yake baada ya kuona hana dalili ya kurudi tena kwenye mchezo huo baada ya kuumia.

Awali alionesha dalili hizo lakini alikuwa sio mtu wa kuutolea macho, lakini aliwahi kufanya mazungumzo na baba yake na akamruhusu kuingia kwenye ushindani kama atakuwa tayari ili aweze kulitangaza jina lake.

Mick mwenye umri wa miaka 20, tayari dunia inamjua sasa kutokana na kitendo alichokifanya wiki moja iliopita kwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya Formula Two ambayo yanajulikana kwa jina la Hungarian Grand Prix.

Ili ni taji lake la kwanza kubwa tangu aanze kushiriki mbio hizo za magari, ameanza kuonesha kufuata nyayo za baba yake ambaye hadi sasa bado yupo kitandani na anaendelea na matibabu.

Inasemekana kuwa, Schumacher alishindwa kuzuia hisia zake baada ya kuona mtoto wake akishinda taji hilo ambalo yeye aliwahi kushinda kama hilo miaka 15 iliopita, hivyo alijikuta kuwa na furaha kubwa akiwa kitandani.

Kitu kingine kikubwa ambacho Schumacher alionekana kuwa na hisia nacho ni baada ya kuona mtoto wake huyo anapigiwa wimbo wa taifa Ujerumani baada ya kutwaa taji hilo mbele ya mama yake Corinna.

Schumacher yeye ilikuwa ni kitu cha kawaida kupigiwa wimbo wa taifa kwa kuwa ametwaa jumla ya mataji 91 katika historia yake, lakini mtoto wake ilikuwa ni mara yake ya kwanza, hivyo anaamini mtoto wake huyo ataliendeleza jina hilo hata kama yeye hatorudi tena kwenye mchezo huo.

Mick kwa upande wake alidai, taji hilo lina maana kubwa kwake kama ilivyokuwa mwaka jana aliposhinda kwenye mashindano ya Formula Three.

“Ni taji muhimu sana kwangu pamoja na familia yangu, ninaamini ninapofanya hivi baba yangu anakuwa na furaha kubwa, kila mmoja anajua hali yake, lakini ushindi huu umemfanya awe na furaha kubwa pale alipo.

“Nitaendelea kufanya hivi ili nizidi kumpa furaha baba yangu pamoja na kujiwekea rekodi yangu katika mchezo huu. nimefurahi kushinda huku familia yangu ikishuhudia.

“Sitaki niishie hapa, lengo langu kubwa ni kuhakikisha ninafanya makubwa zaidi hasa nitakapopata nafasi ya kushiriki michuano ya Formula One kama alivyokuwa anafanya baba.

“Baba amekuwa akinifuatilia kupitia runinga, hivyo nikifanya makosa lazima aniseme kwa kuwa anaangalia mbio za magari kila wakati na anatumia muda wake mwingi kwenye runinga kwa kuwa anapata furaha ya moyo wake,” alisema Mick.

Schumacher anaamini ipo siku atarudi katika hali yake ya kawaida na kuendelea kufurahia mchezo wa Formula One ambao umempa jina kubwa duniani pamoja na utajili alionao.

Familia ya bingwa huo imeweka wazi itaendelea kupambana na hali yake hadi hatua ya mwisho huku wakiamini kila kitu kitakuwa sawa, hawapendi watu kuja mara kwa mara kumuangalia kwa kuwa wanaogopa kusambaza taarifa za hali yake, lakini wenyewe wanadai anaendelea vizuri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles