23.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 10, 2024

Contact us: [email protected]

Michael Urio achaguliwa Naibu Meya Kinondoni

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Diwani wa Kata ya Kunduchi, Michael Urio, amechaguliwa kuwa Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni  baada ya  Josephat Rwegasila kumaliza muda wake.

Urio amechaguliwa kwa kura zote za ndio 21 kutokana na kuwa mgombea pekee katika uchaguzi huo ulifanyika leo Agosti 2024 kwenye Ukumbi wa Manispaa ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Michael Urio (kushoto)akizungumza baada ya kuchaguliwa leo Agosti 20,2024, katikati ni Meya wa Manispaa hiyo, Songoro Mnyonge na kulia ni Msimamizi wa uchaguzi Charles Lawisso.

Akizungumza baada ya kumtangaza  Naibu Meya huyo, Meya wa Kinondoni, Songoro Mnyonge ameahidi kumpa ushirikiano  wa dhati katika kazi zote watakazofanya.

“Urio karibu ufanye kazi, umeahidi utanisaidia naomba unisaidie. Kawaunganishe madiwani wakusaidie,” amesema Songoro.

Diwani wa Kata ya Bweni, Singo Mtambalike akipiga kura wakati wa kumchagua Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Michael Urio leo Agosti 20,2024.

Kwa upande wake, Urio amewashukuru madiwani wenzake na kuahidi kufanya kazi kwa ushirikiano katika kipindi kifupi alichopewa na kufikia malengo waliyokusudia.

“Nikishukuru Chama changu cha Mapinduzi ambacho ndicho kilichonilea, sijawahi kufanya siasa kwenye chama kingine.Nawashukuru sana viongozi wangu kuanzia wa shina hadi Taifa, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan,” amesema Urio.

Miongoni mwa  changamoto ambayo ameahidi kuhakikisha inatatuliwa ni hali ya miundombinu ya barabara hasa katika jimbo la Kawe.

“Jimbo la Kawe tuna changamoto kubwa ya miundombinu ya barabara na toka mvua zimenyesha barabara nyingi hazipitiki,” ameeleza Naibu Meya huyo.

Urio atadumu katika nafasi hiyo hadi Oktoba, 2025

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles