29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, September 19, 2024

Contact us: [email protected]

Michael Johnston: Wanafunzi wana haki ya kufahamu vitu mapema-2

Michael JohnstonMICHAEL MAURUS NA MASHIRIKA (0713 556 022)

SENETA wa Jimbo la Colorado nchini Marekani, Mike Johnston , aliwahi kutoa hotuba matata wakati wa mahafali ya Chuo cha Harvard, Mei 28, 2014, ikiwa ni miaka 14 tangu alipohitimu masomo yake hapo.

Wiki mbili zilizopita tuliwaletea mwanzo wa hotuba hiyo, sasa endelea katika sehemu hii ya mwisho;

Walimu na viongozi wana haki hiyo (kuwapa taarifa wanafunzi wao), tena mapema na mara kwa mara ili waweze kufahamu juu ya maendeleo yao kitaaluma.

Wanafunzi wana haki ya kufahamu maeneo yao na ni wapi wanaweza kujiongeza ili kuwa bora zaidi kwa sababu taarifa hizo ndio mwanga wa safari zetu tulizozichagua.

Haijalishi kama Raquel alichagua kujiunga na Stanford au CU, hilo si swali. Haijalishi Mwalimu amechagua kwenda kujiunga na chuo au kusoma kwa njia ya mtandao, haijalishi iwapo mimi na mke wangu tumechagua kuwapeleka watototo wetu katika shule za lugha maalumuy au kuamini kadri muda unavyozidi kwenda watakuwa wakijifunza.

Kuna watu ambao wanaweza kusapoti moja ya njia hizo mbili, uamuzi wowote kati ya huo unaweza kuwa sahihi. Lakini iwapo tutaamua hivyo bila taarifa za kutosha, tutakuwa tumekosea kitu muhimu mno. Taarifa pekee haziwezi kutibua uamuzi uliofanywa bali hutupa nguvu kwa kuona tunathaminiwa.

Kwa wale wanaopinga kuwa kumfahamu mtoto hakusaidii na kwamba usimsaidie mtoto kusoma ninakubaliana nao. Haki ya kufahamu ndiyo ya msingi kabisa, lakini pia ni hatua muhimu mno.

Kinachotakiwa ni kumpa mtoto fursa ya kujifunza mwenyewe kupitia kile anachokiona au kukisikia kutoka kwa Mwalimu au mzazi wake.

Inafahamika kuwa mtoto anayepewa uhuru zaidi wa kujifunza, huwa mwelewa zaidi kuliko yule aliyebanwa akilazimishwa kushika jambo fulani kwa nguvu zote.

Hivyo sote lazima tujiandae kwa hilo, kutoa haki kwa wanafunzi wetu kujifunza, lakini pia kuwapa taarifa za mara kwa mara ili tuwawezesha kufahamu wametoka wapi na wanaelekea wapi.

Lakini pia, kuna mambo kadhaa ya msingi ambayo ni vema kuyazingatia katika kazi yetu hii ya ualimu na malezi kwa ujumla.

Nguvu ya kuamua na kuchagua

Flavio, kijana ambaye alikuwa akihaha kwa muda mrefu katika miaka yake ya kwanza, hakufahamu ni mambo gani anayoyapendelea zaidi shuleni kwake. Alipendelea zaidi kucheza mpira wa miguu. Kila wakati, ningemuona akiwa nje mkononi akiwa ameshika sigara au akitembea kwa mikogo, lakini muda wote alikuwa kichekesho, mcheshi, mwenye heshima.

Hatimaye alikutana na mwalimu makini ambaye alimwonyesha jinsi alivyojaaliwa, alimwendeleza na kumfanya kuvutiwa na masomo ya madawa.

Baadaye tulimuunganisha na Chuo Kikuu cha Colorado na kwa mwaka mzima alikuwa akitembea huku katika simu yake kukiwa na picha yake. Alisoma kwa bidii mno na kuongeza ufahamu wake na mwisho wa siku kuwa mmoja wa wanafunzi wenye uwezo wa hali ya juu darasani tofauti na alivyokuwa awali, alipokuwa akitumia muda mwingi kwenye uwanja wa mpira wa miguu na kuvuta sigara.

Na baada ya kumaliza chuo, alijiunga na jeshi, kitendo kilichonishangaza sana nikifahamu uwezo wake ungemwezesha kufika mbali kimasomo.

Kuna siku alinitumia ujumbe akisema: “Bwana Johnston, sipendi ujisikie vibaya, niliamua kujiunga na jeshi, nikitaka kulifanyia kitu fulani taifa langu lililonisaidia sana, ninapenda watu kama wewe na Bwana Espinoza ambao mmekuwa muhimili wa mafanikio yangu, kufahamu kuwa nitakuwa wenu siku zote, bila kujali nipo wapi na ninafanya nini.”

Tangu wakati huo, tumekuwa karibu na marafiki wazuri, tukitembeleana na kujuliana hali, akiwa amesafiri katika nchi mbalimbali na hata maeneo tofauti hapa nchini Marekani.

Tunachojifunza hapa, ni kwamba mwanafunzi anaweza kuwa na uwezo mkubwa tu, lakini asijifahamu na mwisho wa siku kupotea iwapo atakosa mtu sahihi wa kumsaidia.

Lakini pia, mwanafunzi anaweza kuwa na uwezo mkubwa, lakini pamoja na kupata mtu wa kumsaidia kufahamu ubora wake, asiwe tayari kukubaliana naye.

Hayo yote ni mambo ya kuzingatia katika kazi hii ya ualimu, lakini iwapo nyote mnasadiki katika taaluma hii.

Tunapokutana na wanafunzi wa aina ya Flavio, ni vema tukafahamu ni jinsi gani tunaweza kukabiliana nao ili kuwasaidia kuchagua na kuamua.

Hayo mnatakiwa kuyafanya mkiwa katika kazi yenu hiyo ya ualimu, mkiwa na rafiki zetu, mashirika, kampuni na sehemu zenu za kazi.

Mungu awabarikli, nawatakieni kila la heri katika mahafali yenu na maisha yenu baada ya kozi hii ya ualimu.

Ahsanteni sana kwa kunisikiliza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles