27.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 7, 2023

Contact us: [email protected]

MIAMI OPEN KURUDISHA HESHIMA YA NADAL?

MARTIN MAZUGWA NA MITANDAO


MARA baada ya kutokuwa katika kiwango bora katika siku za karibuni kutokana na matatizo ya nje ya uwanja, hatimaye mcheza tenisi raia wa Hispania, Rafael Nadal, amerudi katika ubora wake.

Nadal alizaliwa Juni 3, 1986 katika kitongoji cha huko Manacor, Mallorca, nchini Hispania ni moja kati ya nyota wenye uwezo mkubwa katika mchezo wa tenisi.

Mnamo Aprili 2002, akiwa na miaka 15 na miezi kumi, aliweka rekodi ya kuwa mchezaji mdogo kushiriki mashindano ya mchezo wa tenisi.

Nadal aliyekuwa akishika nafasi ya 762 katika viwango vya ubora, mchezo wake wa kwanza alicheza na Ramon Delgado alioshinda na kuweka rekodi ya kushinda mchezo wake wa kwanza katika mchezo huo.

Nyota huyo mwenye urefu wa futi 6-1 pamoja na uzito wa 188, amekuwa mwiba katika mchezo wa tenisi tangu alipoanza kuucheza ambapo amefanikiwa kubeba mataji lukuki.

Mkali huyo amepata ushindi wake wa kwanza msimu huu wa mashindano ya Miami Open pale alipomshinda Dudi Sela, raia wa Israeli.

Katika mchezo huo alishinda kwa seti 6-3 na 6-4, huku akikiri kupata upinzani mkubwa kutoka kwa raia huyo wa Israeli ambaye amekuwa katika kiwango bora hivi sasa.

Baada ya mvua kubwa na hali mbaya ya hewa katika uwanja wa Crandon Park, Nadal alisema kuwa: “Ulikuwa mchezo mgumu lakini nilijitahidi kupata ushindi,” alisema.

“Mashindano haya ni mashindano magumu na kitu chochote kinaweza kutokea.”

“Nafikiri nitakuwa na wiki nzuri mara baada ya kupata ushindi huu nahitaji kufanya mazoezi kwa nguvu zaidi ili kurudi katika ubora wangu,” alisema.

Nadal anatarajia kuingia katika vitabu vya rekodi ikiwa atashuka uwanjani dhidi ya Mjerumani, Philipp Kohlschreiber, ambapo atakuwa anatimiza michezo 1,000 tangu alipoanza kucheza mchezo wa tenisi.

Mkali huyo atakumbana na wakati mgumu kutoka kwa Mjerumani huyo ambaye mchezo uliopita ametoka kupata ushindi dhidi ya Taylor Fritz ambapo alimbwaga kwa seti 7-5, 3-6, 7-6.

Mkali huyo ameshushwa na hasimu wake, Roger Federer, katika viwango vya ubora kwa nafasi moja kutoka nafasi ya sita hadi ya saba.

Nadal ambaye hadi sasa anashikilia mataji 14 ya Gland slams, ni nyota wa kuchungwa zaidi katika mashindano haya yanayoendelea nchini Marekani.

Mwaka 2017 umeanza vibaya kwa nyota huyo mara baada ya kuingia kwa tabu hatua ya robo fainali ya Australian Open mara baada ya kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Milos Raonic katika seti ya tatu.

Lakini licha ya kufika hadi hatua ya fainali aliambulia patupu mara baada ya kupoteza mbele ya Mswisi Federer.

Huenda mashindano haya yalimuuma zaidi Nadal mara baada ya taji hilo kubebwa na hasimu wake, Federer, aliyeshinda taji hilo tangu mwaka 2014 alipofanya hivyo.

Lakini pia ulikuwa ni mchezo wa kisasi zaidi kwani mara ya mwisho kumshinda nyota huyo ilikuwa 2007 katika mashindano ya Wimbledon.

Nyota huyo mwenye medali mbili za dhahabu alizozipata katika mashindano ya Olimpiki mwaka 2008 nchini Beijing pamoja na 2016 nchini Rio de Janeiro nchini Brazil.

Mbali na medali hizo pia nyota huyo ana taji moja la Australian Open aliloshinda mwaka (2009) pamoja na mataji tisa ya

French Open aliyoshinda miaka ya (2005, 2006, 2007, 2008, 2010, 2011, 2012, 2013, 2014).

Mataji mengine anayoshikilia nyota huyo ni pamoja na Wimbledon aliloshinda mara mbili mwaka (2008, 2010) pamoja na US Open aliyoshinda mara mbili (2010, 2013).

Lakini pia mkali huyo mwenye rekodi nzuri anashikilia mataji manne ya Davis Cup aliyoshinda miaka ya (2004, 2008, 2009 pamoja na 2011).

Msimu uliopita ulikuwa wa mafanikio kwa nyota huyo mara baada ya kunyakua taji la Mubadala na kisha kubeba medali ya dhahabu nchini Brazil.

Nadal ataweza kurudi katika ubora wake na kuendelea kunyanyua mataji mara baada ya kushindwa kuongeza taji la Gland slams mwanzoni mwa mwaka huu, ni jambo la kusubiri na kuona.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,885FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles