24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

MIAKA 70 YA JANGA lA WANANCHI WA PALESTINA

Mojawapo ya Kambi za Wakimbizi wa ipalestina ambao kwa miaka 70 wamekuwa wakipigania haki ya kurejeshewa ardhi zao katika kanda wa Gaza na maeneo mengine.

EAST JERUSALEM, PALESTINA     |


WANANCHI wa Taifa la Palestina wanatarajiwa kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 70 ya Nakba ifikapo Mei 15 mwaka huu, ili kuendeleza mapambano kabambe ya kurudisha haki zake msingi na thabiti za kizalendo.

Nabka ni janga, ambalo liliwakuta baada ya kupokonywa ardhi yao na kuchukuliwa na Israel. Wapalestina bado wanaamini katika mapambano na mshikamano wa kuondoa athari na matokeo ya uonevu ambao bado upo katika nyanja zote za maisha yao ya kila siku.

Mapambano ya kitauifa wanayoshikilia Palestina ni kwaajili ya ukombozi wa kizazi chao na kijacho ili kuthibitisha malengo na shabaha yake hata kama ni kwa muda mrefu.

Licha ya uadui wa utekaji na uhalifu wake unaoendelea katika ardhi yao na watekaji kuungwa mkono na Marekani chini ya Rais Donald Trump bado Plaestina imesimama imara.

Uamuzi wa Israel, kuhamishia makao makuu mjini Jeruselemu pamoja na mwitiko wa Marekani kuhamishia mjini humo ubalozi wake ni dhihirisho la la ukiukwaji sheria za kimataifa.

Kwa mantiki hiyo Palestina inayo haki na uhuru wa kuwakumbusha wananchi wake popote pale walipo kwa nguvu za kizalendo na taasisi zake huikumbuka kumbukumbu hiyo.

Aidha, mwaka huu kunatarajiwa kushuhudiwa mabadiliko makubwa na muhimu kwani inaenda sambamba na safari kubwa ya kurejea iliyoanza tangu wiki kadhaa kwenye mipaka ya kihistoria na ukanda wa Gaza.

Makumi ya watu wamekufa mashahidi na maelfu wamejeruhiwa. Kilele chake cha maadhimisho hayo kitakuwa Mei 14 -15 ikiwa ni ushahidi tosha kwa wananchi wa Palestina kushikama na kutimiza malengo na haki zake vijijini kwao na mali zao pamoja na kusimamisha taifa lake la Palestina.

Ukweli msimamo wa Marekani na hatua iliyoichukua mnamo Januari mwaka huu, wa kupunguza msaada wake kwa Kuhudumiwa Wakimbizi Palestina (UNRWA) kwa kiasi cha dola za kimarekani milioni 65. Uamuzi huu kwa taifa letu umezua hofu kwa suala la wakimbizi kwa kujaribu kulifuta na kuliweka hatarini kwa masilahi ya msimamo mkali wa serikali ya Israel ambao unajitahidi kwa nguvu zote kulitokomeza suala hilo.

Lengo kukausha vyanzo vya misaada ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwasaidia na kuwahudumia wakimbizi wa Palestina (UNRWA), hadi kufikia kuliondoa kikamilifu.

Nakba lililowakumba Wananchi wa Palestina, ambalo limepelekea kuhamishwa maelfu ya wapalestina, hasa kile kilichojumuishwa na “Mpango wa Dalet” uliopitishwa na Shirika la Kizayuni mwanzoni mwa mwaka 1948 na kuachiwa utekelezaji wake Haganah kwa muongozo wa uwazi, kama vile kuua, kutisha, kuzingira miji na vijiji vya Palestina, kuchoma nyumba na mali, kuzika mabomu katika vifusi ili kuwazuia wenyeji kurejea katika nyumba zao kama ilivyotokea mjini Deir Yassin mnamo Aprili 9, 1948.

Hii ni pamoja na kuvunjwa na kuteketezwa miji na vijiji 531, kuhamishwa wapalestina laki nane (8) waliofanywa kuwa ni wakimbizi katika nchi yao, ni sawa waliokuwa katika ardhi ya mwaka 48, Ukingo wa Magharibi au Ukanda wa Gaza.

Palestina wanakumbuka kuwa nyaraka na tafiti za kielimu, dalili za wazi zenye kuthibitisha ukweli wa maelezo ya Palestina na uongo wa maelezo ya kiisraeli. Mthalani nyaraka rasmi za Israeli zilizoonesha aliyoyasema Waziri Mkuu wa zamani wa Israeli ambaye ni kiongozi wa chama cha Herut na baadae chama cha Likud, gaidi “Menachem Begin”, aliyesema: Lau si mji wa Deir Yassin (mauaji yaliyopoteza kiasi cha wapalestina 320 waliokuwakaribu na Jerusalemu) asingekuwepo Israeli.

Kama inavyowezekana kupata muongozo kupitia maandiko ya wanahistoria wengi wa Israeli waliokuwa maarufu, mfano “Ilani Pappe” kuhusu utokomezaji wa kikabila nchini Palestina, pia “Benny Morris” kuhusu ule mpango uliojulikana kwa jina la “Mpango wa Dalet”, kuwa ni uongo wa kuondoka kwa hiari kwa Wapalestina.

Hakika kutaja ukweli huu na kuweka wazi uovu wa vikundi vya kizayuni na dola ya Israeli na kuzionesha kwa ulimwengu mzima, hakulengi kuandika ukweli wa kihistoria tu kwa malengo ya kimaarifa na kinadharia, bali hilo ni jambo linalohudumia mpango wetu wa kitaifa na malengo ya mapambano yetu ya sasa, katika kudai hakuna kuondoa dhulma kwa wananchi wa Palestina, pia kulaani udhalimu na ubaguzi wa kizayuni.

Pia kudhihirisha majukumu ya dola tekaji katokana na dhuluma ya kihistoria dhidi ya wananchi wa Palestina, vilevile kutilia mkazo majukumu ya jamii ya kimataifa katika kukomesha dhulma na haki ya wananchi wetu ya kufikia katika ufumbuzi wa kisiasa unaowiana iliyopo katika misingi ya haki na maazimio ya kisheria ya kimataifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles