25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Miaka 60 ya Uhuru| Prof. Kabudi aanika mafanikio ya miaka 60 nyanja ya Sheria na Katiba

*Asema mikutano siasa haijazuiliwa bali inaratibiwa…

*Majadiliano yanaendelea umri sahihi wa binti kuolewa

*Sheria 154 zatafasriwa kwa Kiswahili

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

WAZIRI wa Sheria na Katiba, Profesa Paramagamba Kabudi ameeleza mafanikio ambayo imeyapata Wizara hiyo ndani ya miaka 60 ya uhuru wa Tanzania Bara huku akidai mikutano ya siasa haijazuliwa bali inaratibiwa na imewekewa utaratibu wa kufanyika ambapo amedai jambo lolote halifanyiki bila ya kufuata utaratibu.

WAZIRI wa Sheria na Katiba, Profesa Paramagamba Kabudi, akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dodoma.

Akizungumza leo, Alhamisi Novemba 18,2021 na Waandishi wa Habari jijini Dodoma wakati akieleza mafanikio ambayo Wizara hiyo imeyapata ndani ya miaka 60 ya uhuru wa Tanzania Bara, Waziri Kabudi amesema mikutano ya siasa haijazuliwa bali inaratibiwa na imewekewa utaratibu wa kufanyika.

“Na hakuna jambo lolote ambalo halifanyiki bila utaratibu wengi tunaisoma sura ya pili ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa haki za binadamu bila ya kosoma inara ya 30 ibara ya 30 imeweka mipaka katika kufaudu uhuru wako ni kweli tunauhuru wa kuabudu,” amesema.

MAJADILINO YANAENDELEA UMRI SAHIHI WA MTOTO WA KIKE KUOLEWA

Kuhusu sheria ya ndoa ya mwaka 1971 kuwa na matatizo, Waziri Kabudi amesema bado wanaendelea mashauriano na wadau mbalimbali kwa maelekezo ya Bunge ili waone jinsi nzuri ya kutekekeza maombi au mahitaji ya umri wa mtoto wa kike kuolewa uwe ni miaka 18.

“Niwakumbushe watanzania sheria hii ni ya kimapinduzi,sheria hii haikuungwa mkono na baadhi ya madhehebu ya Dini, Watu watatu walisimama imara ili sheria hiyo ifanye kazi, Mwalimu Nyerere, Rashid Kawawa na Mama Sophia Kawawa haikuwa rahisi sheria hii

“Tumeuandaa muswada na kuupeleka bungeni kamati ya bunge kupitia muswada huo imeiachia serikali iendelee na mashauriano na wadau mbalimbali kwahiyo sasa tunaendelea mashauriano na wadau mbalimbali kwa maelekezo ya Bunge ili baadae tuone njia nzuri zaidi ya kutekeleza maombi au mahitaji ya umri wa mtoto wa kike kuolewa iwe umri wa miaka 18,”amesema.

LUGHA YA KISWAHILI NA SHERIA 154 KUTAFSIRIWA

Aidha,Prof Kabudi amesema mpaka sasa wizara hiyo imefanikiwa kutafsiri sheria 154 na kuzipeleka katika lugha ya kiswahi huku akisema kuwa kazi hiyo bado inaendelea.

“Kwa hiyo mpaka sasa sheria 154 zimetafsiri katika lugha ya Kiswahili kwa hatua ya rasimu ya kwanza ,na zoezi la kutafsiri linaendelea ,na ni matarajio yetu ndani ya miaka miwili ijayo tutakuwa tumepiga hatua kubwa katika zoezi la kutafsiri sheria.

“Kazi kubwa tuliyonayo sasa ni kutunga kitabu cha histilahi za kisheria kwa Kiswahili ili kusiwe na tafsiri za mitaani katika kutafsisri maneno ya kisheria ya kingereza ,haya yote ni mafanikio makubwa sana,” amesema Prof. Kabudi.

MATUMIZI YA LUGHA YA KISWAHILI KATIKA MAHAKAMA

 Profesa Kabudi amesema ,katika kipindi chote katika mahakama za mwanzo, mahakama za Rufani Kiswahili kimekuwa kikitumika.

Sehemu ya Waandishi wa Habari.

 “Kanuni za mahakama ya rufani zilizopitishwa wakati wa Jaji Mkuu Augustino Ramadhani, ziliruhusu matumizi ya Kiswahili katika mahakama ya rufani,kwa hiyo katika Mahakama za mwanzo Kiswahili daima kimekuwa kikitumika na katika mahakama ya rufani wewe unayepeleka shauri ulikuwa na hiari kutumia Kiswahili au kingereza.

“Kwa hiyo maamuzi yaliyofanywa ya mabadiliko ya sheria mwaka jana ni kukifanya Kiswahili kuwa ni lugha ya kutunga sheria maana yake sasa sheria zitatungwa na kuandikwa kwa lugha ya Kiswahili.

“Na nipende kuwaarifu kuwa Shirika la Elimu,Sayansi na Utamaduni UNESCO sasa limetangaza kila Julai 7 ya kila mwaka itakuwa siku ya lugha ya Kiswahili,” amesema Prof. Kabudi.

UKOMAVU KISIASA.

Waziri Kabuni amesema: “Tunangia miaka 60 ya uhuru tukiwa tumeidhihirishia dunia ukomavu wetu wa kisiasa na umadhubuti wa ukatiba kama tulivyodhihirisha baada ya msiba wa aliyekuwa  Rais John Magufuli kutokea na Rais wa awamu ya sita Samia Suluhu Hassan na  kuapishwa kwa utulivu na amani ,taifa letu linazidi kusonga mbele.”

Pia Profesa Kabudi amesema  mafanikio mengine yaliyopatikana ni pamoja na kuwa  Taifa lililoingia katika uchumi wa kati miaka mitano kabla ya muda uliokadiriwa  katika kipindi kigumu cha mlipuko  wa janga la UVIKO 19.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles