27.5 C
Dar es Salaam
Sunday, December 3, 2023

Contact us: [email protected]

Miaka 45 ya CCM; DC Ileje aagiza upandaji miti

Denis Sinkonde, Songwe

MKUU wa wilaya ya Ileje mkoani Songwe Anna Gidarya ameagiza kila kaya na taasisi wilayani hapo kupanda miti huku akipiga marufuku wananchi kufanya shughuli za kibinadamu pembezoni mwa vyanzo vya maji.

Anna ametoa tamko hilo katika jana maadhimisho ya miaka 45 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Amezielekeza kaya na Taasisi zote wilayani hapo kuhakikisha ndani ya miezi miwili miti iliyopandwa inaongezwa, ili kulinda mazingira na kulifanya zoezi hilo kuwa endelevu.

Katibu wa CCM Wilaya ya Ileje, Hassan Lyamba akipanda mti.

“Wananchi wanapaswa kulinda vyanzo vya maji na kupanda miti ili kuondoa tatizo la uhaba wa maji na kulinda makazi yao ambayo huathiriwa na upepo,” amesema Anna.

Mwenyekiti wa CCM wilayani Ileje, Hebron Kibona amesema, madhimisho hayo yanapaswa kuendelezwa kwa kuwaenzi waasisi wetu kwa kuhakikisha taifa linapata maendeleo.

Akizungumza katika maadhimisho hayo chifu wa tarafa ya Bulambya wilayani hum,o Simime Mwampashi, amewataka wananchi kujijengea tabia ya kupanda miti iwe endelevu ili kutunza uoto wa asili .

Maadhimisho hayo ambayo kilele chake kitaifa ni Februari 5, mkoani Mara, yanaenda sambamba na kugawa madaftari, kalamu, mafuta ya kupaka na sukari kwa wanafunzi wa shule za msingi wanaoishi mazingira magumu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles