23.7 C
Dar es Salaam
Thursday, September 28, 2023

Contact us: [email protected]

Miaka 36 Tanzania bila medali Olimpiki

BayiNA WINFRIDA NGONYANI,DAR ES SALAAM

MICHEZO ya 31 ya kimataifa duniani ya Olimpiki itaanza rasmi Agosti 5 mwaka huu hadi 21 katika jiji la Rio de Jeneiro nchini Brazil.

Tanzania inakwenda kushiriki michezo mitatu tu kati ya 28, ambapo safari hii mchezo wa ngumi ambao umekuwa ukifanya vizuri kimataifa hautakuwa na mwakilishi baada ya kushindwa kufuzu.

Katika michezo ya mwaka huu, Tanzania inawakilishwa na watu 12, saba wakiwa wachezaji na watano ni viongozi.

Tayari timu hii imejiandaa kwa staili tofauti tofauti, ambapo wanariadha Alphonce Felix Simbu, Saidi Juma Makula, Fabiano Joseph Naasi na Sara Ramadhani Makera wao walikuwa  kambini Arusha.

Wakati washiriki wa kuogelea wao kambi yao ilikuwa nje ya nchi, ambapo muogeleaji Hilal Hemed yeye alikwenda kujikoki huko Dubai wakati Magdalena Ruth Alex, kwa upande wake alikwenda kujifua huko Adelaide, Australia.

Mchezaji atakayeiwakilisha nchi kwa upande wa  judo, Andrew Thomas Mlugu, yeye alikuwa akifanya mazoezi bila kukaa kambini kutokana Cham Cha Judo Tanzania JATA, kushindwa kumwezesha kutokana na ukata unaokikabili chama hicho.

Mlugu alikuwa akijiandaa kwa udhamini kutoka kwa  Kocha wake, ambaye ataongozana nae, Zaidi Hamisi na mlezi wa chama hicho.

Licha ya wanamichezo hawa kwenda huko Brazil, kumekuwa na malalamiko mbalimbali ya wachezaji kudai kuwa, maandilizi yao kiujumla ni ya kawaida kulingana na michezo yenyewe ambayo ni ya kimataifa na yanashirikisha wanamichezo mbalimbali duniani.

Yamekuwa ya kawaida kwa maana kwamba, vyama vinavyowasimia vimekuwa havina fedha jambo ambalo kwa namna moja ama nyingine limewasababishia kutojiandaa vema.

Ikumbukwe kuwa, nchi inakwenda kushiriki katika michezo hii ikiwa haijapata medali tangu mwaka 1980, wakati michezo hiyo ilipofanyikia Moscow, Urusi, ambapo Filbert Bayi na Suleiman Nyambui walipata medali za fedha.

Bayi alitwaa medali hiyo kutoka katika mchezo wa mbio za meta 3000 kuruka viunzi, wakati Nyambui yeye alifanya vema  katika mbio za meta 5000.

Hakika nchi kukaa miaka yote hiyo bila kuvuna chochote katika michezo hiyo ni jambo la kusikitisha na la kukatisha tamaa.

Niwazi kuwa, wakati umefika sasa kwa serikali kuliangalia suala hili kwa jicho la kipekee, kwa kuwandaa wanamichezo wengi zaidi na katika michezo mingi zaidi, ili tusirudi nyumbani mikono mitupu.

Michezo hii ni muhimu kwani nchi zinazoshiriki zinajitambulisha kimataifa, pia wachezaji wapata fursa ya kukutana na wachezaji wenzao na kujifunza mambo mbalimbali.

Mfano nzuri ni Kenya, ambao wao mwaka huu, wanapaleka wanamichezo 50 kushiriki katika michezo hiyo, kwa namna fulani, hii inaweza ikawasaidia kujipatia medali kadhaa kutokana na idadi hii kubwa ya wachezaji.

Nafasi ya kufanya vema katika michezo hii ipo, endapo serikali itasapoti vyama vya michezo nchini kwa kuvipa ruzuku, ikiwa ni pamoja na kuwaandaa wanamichezo mbalimbali wanaoshiriki michezo ya kimataifa.

Nakubaliana kabisa na maneno aliyoyatoa mwanariadha wa zamani Bayi, ambaye sasa ni Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) aliyesema, Tanzania inakwenda kushiriki na si kupata medali.

Aibu ya kushindwa kupata medali katika michezo hii inaweza kufutwa kama wanamichezo wataandaliwa vema, tena mapema mfano maandalizi ya Olimpiki ya mwaka 2020 yaanze sasa.

HISTORIA YA OLIMPIKI.

Michezo ya hii ilianzishwa miaka 3000 iliyopita, katika mji wa Olimpia, kusini magharibi mwa nchi ya Ugiriki.

Tangu kuanzishwa kwake hakuna nchi hata moja ya Afrika ambayo imeweza kufanikiwa kuandaa michezo hii, wakati Marekani wao wakiongoza kuandaa michezo hii mara 8.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,745FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles