25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Miaka 30 jela kwa kumbaka, kumpa mwanawe ujauzito

Na HADIJA OMARY-LINDI

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Lindi, imemuhukumu mkazi wa Kijiji cha Mahiwa, Kata ya Nyangao, Maulid Salum (25) kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na makosa mawili likiwemo la kumbaka na kumpa ujauzito mwanawe wa kufikia (13) ambaye ni mwanafunzi.

Mshtakiwa huyo pia atachapwa viboko 12 pia atatakiwa kumlipa mlalamikaji fidia ya Sh milioni 2.

Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Maria Batraine, baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka.

Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo mshitakiwa alipewa nafasi ya kujitetea ambapo aliomba mahakama itekeleze majukumu yake kama sheria inavyoelekeza kwa sababu yameshatokea hivyo hana la kujitetea kwa hilo.

Baada ya maelezo hayo Mwanasheria wa Serikali, Godfrey Mramba, akaiomba mahakama kumpa mshtakiwa adhabu kali ili iwe fundisho kwake na wengine walio na tabia ya aina hiyo.

Alidai kitendo kilichofanywa na mshtakiwa ambaye ni baba mlezi si cha kiungwana na hakiwezi kuvumilika kwani kimekatisha ndoto za mtoto huyo aliyekuwa akisoma shule ya msingi (jina linahifadhiwa).

Katika kosa la kubaka, kumpa mimba na kukatisha masomo ya mwanafunzi huyo mahakama ilimuhukumu mshtakiwa huyo kifungo cha miaka 30 gerezani pamoja na kuchapwa viboko 12 na atakapomaliza kutumikia adhabu yake amlipe mlalamikaji fidia ya Sh milioni 2.

Awali ilidaiwa mahakamani hapo kuwa siku isiyofahamika Machi mwaka huu mshtakiwa akiwa ni baba wa kufikia alimbaka mtoto huyo na kumpa ujauzito.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles