29.8 C
Dar es Salaam
Sunday, September 15, 2024

Contact us: [email protected]

MI CASA X YouNotUs ndani ya “CHUCKS”

Na Mwandishi Wetu

KUNDI mahiri la muziki kutoka nchini Afrika Kusini, Mi Casa kwa kushirikiana na Kundi la YouNotUs kutoka Berlin nchini Ujerumani, wamezindua video ya wimbo wao mpya wa Chucks.

Mapokeo mazuri ya wimbo huo ambao ‘audio’ yake iliachiwa wiki mbili zilizopita katika nchi mbalimbali duniani, yamekuwa makubwa kuliko matarajio ya wasanii hao, hususan katika idadi ya watu waliosikiliza kupitia majukwaa mbambali ya muziki (streaming).

Video ya wimbo huo, imerekodiwa na wasanii wa makundi hayo makubwa duniani, wikiendi iliyopita nchini Namibia.

Dairekta wa video hiyo, ni Marvin Ströter kutoka nchini Ujerumani na imerekodiwa katika mitaa ya Jiji la Windhoek, Walvis Bay na Swakopmund na imejumuisha ndani yake mandhari nzuri za nchi ya Namibia pamoja na wasanii hao kujichanganya na wenyeji.

Namibia ilichaguliwa kuwa sehemu ya kurekodia video hiyo kutokana na masharti rahisi kuhusu maambukizi ya Virusi vya Covid 19 lakini pia mandhari ya nchi hiyo, yana uwiano mkubwa kati ya kitu kinachoimbwa na mazingira yanayooneshwa kwenye video, ambapo ujumbe mkubwa uliopo ndani ya wimbo huo ‘sote tutakufa kwa hiyo ishi maisha yako kwa ubora wa juu unapoweza na kamwe usikate tamaa.’

Mandhari nzuri kama majangwa, bahari, majengo makubwa na tambarare za Namibia, zimeifanya video hiyo kuwa na ubora wa hali ya juu.

Kwa kutumia mandhari hizo na mashairi yaliyomo ndani ya wimbo wenyewe, yamelifanya Kundi la Micasa kuonesha ubora wa hali ya juu katika video hiyo ya Chucks, wakisambaza upendo wao katika medani za kimataifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles