22.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Mhasibu Ushirika mahakamani kwa uhujumu uchumi

Na Derick Milton, Simiyu

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, imemfikisha mahakamani Mhasibu Msaidizi Idara ya Ushirika Halmashauri ya Wilaya hiyo, Daudi Makoye kwa makosa ya uhujumu uchumi.

Ofisa huyo amefikishwa leo Machi 29, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Simiyu na kusomewa Mashtaka mawili yanayomkabili ambayo ni kuchepusha mali ya Serikali ikiwa kwa madhumuni yasiyohusiana na ilivyokusudiwa.

Kosa la pili ni Ubadhilifu na ufujaji wa mali kinyume na kifungu cha 28 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa No. 11 ya Mwaka 2007.

Mbele ya Hakimu mkazi wa Mahakama hiyo, Martha Mahumbuga, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Josephat Jankila ameelezea Mahakama kuwa Mshtakiwa alitenda makosa hayo tarehe 23/09/2021 katika wilaya ya Maswa.

Mwendesha Mashtaka huyo amesema kuwa Mshtakiwa akiwa mwajiriwa wa halmashauri ya Maswa kama Mhasibu msaidizi wa halmashauri idara ya Ushirika alifanya ubadhilifu wa Sh 5,524,000,200.

Amesema Mtumishi huyo alitumia fedha hizo kwa matumizi yake binafsi wakati akijua kuwa ni mali ya umma, fedha ambazo zilitolewa na Amcos ya WITAMILYA iliyoko kwenye wilaya hiyo kwa ajili ya kulipa kodi Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) pamoja na Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Simiyu (SIMCU).

Aidha, katika maelezo ya kosa la pili, Mwendesha Mashtaka huyo amesema kuwa Mshtakiwa alichepusha fedha hizo kwa madhumuni yake binafsi kinyume na kifungu cha 29 cha sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa No. 11 ya Mwaka 2007.

Mara baada ya kusomewa makosa hayo, Mshtakiwa alikana makosa yote mabapo Hakimu ameiharisha kesi hiyo hadi April 24, 2022 itakapokuja kwa ajili ya kusoma hoja za awali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles