31.2 C
Dar es Salaam
Saturday, December 2, 2023

Contact us: [email protected]

Mhandisi aridhishwa mradi wa maji

Na Mohamed Saif – Busega

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Emmanuel Kalobelo amesema ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi wa maji katika mji mdogo wa Lamadi  wilayani Busega mkoani Simiyu ambao utekelezaji wake umefikia asilimia 93.

Aliyasema hayo mwishoni mwa wiki, wakati wa ziara ya mradi na washirika wa maendeleo wanaowezesha utekelezaji wa miradi ya maji kupitia programu ya uboreshaji wa huduma ya majisafi na usafi wa mazingira ijulikanayo kama LV Watsan ambao ni Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB) na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD).

Kalobelo alisema amefarijika kushuhudia hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa mradi na aliongeza kuwa hadi kufikia Agosti, mwaka huu utakuwa umekamilika.

Alisema Lamadi ni mji ambao kwa muda mrefu ulikuwa na ukame na kwamba mradi huo ni mkombozi kwa wananchi wa maeneo hayo na unadhihirisha matumizi sahihi ya Ziwa Victoria.

Aliwataka wananchi wanaozunguka Ziwa Victoria kuhakikisha wanatunza mazingira, hasa ikizingatiwa manufaa wanayoyapata ni makubwa kwao na kwa vizazi vijavyo.

Kwa upande wake, Mratibu nradi kutoka EIB, Raoul Pedrazzani alisema miradi inayotekelezwa chini ya LV Watsan, imeonesha mafanikio makubwa na aliipongeza Mamlaka ya Maji Mwanza (Mwauwasa) ambayo inajukumu la kusimamia miradi hiyo kwa niaba ya Wizara ya Maji kwa usimamizi mahiri wa utekelezaji wake.

Naye Ofisa Miradi kutoka AFD, Clement Kivegalo alisema wameridhishwa na hatua ya utekelezaji wa mradi na kwamba AFD itaongeza udhamini kadiri itakavyohitajika kufanya hivyo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Busega, Tano Mwera ambaye alikuwa mwenyeji wa ugeni huo wilayani hapo, alisema mradi unatarajiwa kuleta mabadiliko makubwa kwenye wilaya na hususan katika mji wa Lamadi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mwauwasa, Anthony Sanga alisema mradi huo unafadhiliwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia mia moja kupitia mkopo wa masharti nafuu kutoka EIB na AFD kwa gharama ya Sh bilioni 12.83.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles