24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

MGONJWA WA KWANZA WA ‘SIKOSELI’ APONA

CHIGACO, MAREKANI

KAMA wewe au mtu yeyote unayemfahamu anasumbuliwa na ugonjwa wa selimundu au kama unavyojulikana kwa lugha ya kitaalamu sickle cell, unatakiwa kuwa na matumiani kuwa atapona.

Iesha Thomas, ambaye alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa huo kwa muda mrefu, ni mgonjwa wa kwanza kupatiwa matibabu na kupona kabisa. Hii ni hatua kubwa mno kufikiwa katika matibabu ya ugonjwa huo.

Ugonjwa wa selimundu umekuwa ni janga linaloathiri takribani raia mmoja kati ya 500 wa Marekani wenye asili ya Afrika, lakini habari njema ni kwamba, ugonjwa huo sasa umepatiwa ufumbuzi na kuweza kutokomezwa.

Iesha, mwenye umri wa miaka 33, alikuwa akiishi na kusumbuliwa na ugonjwa wa selimundu ambao ulimfikisha katika kipindi kigumu zaidi maishani mwake.

Ugonjwa huo uliharibu sehemu kubwa ya maisha yake tangu alipojifungua mtoto wa kike, na kusababisha kubadilishwa damu pamoja na kubadili nyama za paja kutokana na kuvunjika kwa mifupa.

Ugonjwa huo unaweza kusababisha maumivu makali. Seli nyekundu za damu zinabeba oksijeni mwilini.

Seli nyekundu za damu za kawaida ni za mviringo na laini na zinatiririka kirahisi ndani kwenye mabomba ya damu. Zina umbo la mviringo.—

Watu wengine wana seli nyekundu za damu ambazo ni ngumu na zenye umbo la mundu au la hilali.—

Seli zenye umbo la mundu zinaweza kufungwa pamoja na kuziba mabomba madogo ya damu kama mtu anaumwa, anakuwa baridi sana, au anapoteza maji.

Wakati mabomba ya damu yanaziba, oksijeni kidogo zaidi hufikia sehemu ile ya mwili. Mabomba ya damu yaliyozibwa yanaweza kusababisha maumivu, maambukizo na hasara ya viungo vya mwili. Hii inakuwa shida kubwa kama mapafu au ubongo ukiathirika.

Lakini sasa mtu wa kwanza kupona ugonjwa huo ni Iesha Thomas.

“Ninachotaka ni kupumzika nyumbani na binti yangu iwe mchana au usiku,” alisema Thomas.

Madaktari kutoka Hospitali ya Chuo cha Illinois walipitia njia mbalimbali za kupata dawa za kutibu ugonjwa huo kwa kutumia dozi ndogo kabla ya kupandikiza seli. Njia hizo zinaruhusu seli zilizopo ndani ya mifupa kuishi kwa msaada wa mpya zilizowekwa.

Lengo kubwa la upandikizaji ni kwa seli hizo kuingia ndani na kurekebisha mfumo wake ili uwe wa kawaida pamoja na kufanya kazi na seli nyekundu.

Madaktari wamempa pongezi nyingi Iesha Thomas na kusisitiza kuwa, watu wote wanaougua ugonjwa huo wanatakiwa kufuatia njia aliyotumia ili kuponywa.

 

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles