26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 27, 2021

MGOMO WA MABASI KUANZA LEO NCHINI

Na TUNU NASSOR-DAR ES SALAAM


CHAMA cha Wamiliki wa Mabasi nchini(TABOA) kimesema mgomo usiokuwa na kikomo utaanza rasmi kesho.

Juzi TABOA kilitangaza mgomo usiokuwa na kikomo unaolenga kupinga sheria zilizotungwa na Mamlaka ya Udhibiti wa usafiri wa nchi kavu na majini(SUMATRA)ambazo zinadaiwa kuwa na vifungu kandamizi vinavyoweza kutishia ustawi wa biashara hiyo nchini.

Akizungumza na MTANZANIA Katibu Mkuu wa Taboa, Enea Mrutu alisema wanawaagiza mawakala leo kutowakatia tiketi abiria ili kuepuka usumbufu utakaojitokeza.

Alisema sheria zinazolalamikiwa ni pamoja na ile ya leseni na usafirishaji sura ya 317namba 11(6)ambacho kina kipengele cha kutaifisha magari kwa makosa ya kibinadamu.

“Sheria inayotaka kuitaifisha gari (forfeitureof motor vehicle)ifutwe kwa sababu katika hali ya kawaida adhabu hiyo ni kubwa ukilinganisha na thamani ya gari na makosa mengi yanayotajwa ni ya kibinadamu,” alisema Mrutu.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
163,388FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles