27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

MGOMBEA URAIS AKAMATWA KWA KUTAKA KUJIUA KENYA

NAIROBI, KENYA


POLISI wanamshikilia mgombea urais binafsi Peter Solomon Gichira kwa kujaribu kujiua baada ya ombi lake la kugombea urais kukataliwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC).

Gichira, ambaye alifanikiwa kufungua kesi mahakamani kubatilisha baadhi ya sheria zilizowekwa na IEBC kwa wagombea binafsi, alijaribu kujirusha kutoka gorofa ya sita ya Jengo la Anniversary Towers juzi jioni.

Ofisa mwandamizi wa Polisi jijini hapa, Robinson Thuku alisema Gichira alikuwa kwenye ofisi za IEBC kuangalia maendeleo ya uteuzi wake wa kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa Agosti 8.

Thuku alisema wakati alipobaini IEBC imekataa ombi lake, alivunja dirisha la gorofa ya sita na kujaribu kujirusha kabla ya maofisa wawili kumuwahi kwa kumwokoa na kumkamata.

Thuku alisema mwanasiasa huyo atafikishwa mahakamai leo kwa mashitaka ya kujaribu kujiua na kuharibu mali.

Hata hivyo, polisi wamekataa kumwachia kwa dhamana wakisema wanamlinda, wakihofia kumwachia kunaweza kuwa tiketi ya kumruhusu kutekeleza mpango wake wa kujiua.

Ndugu zake na mgombea wake mwenza Kelly Watima, wamepiga kambi polisi kujaribu kutafuta njia ya kumtoa kwa dhamana.

Watima alidai Gichira amekuwa akiishi kwa vitisho na ukandamizaji tangu alipotangaza mpango wake wa kuwania urais.

Naye Menaja Kampeni wa Gichira, David Muriuki alisema alifuatilia IEBC kuhusu maendeleo ya ugombea wa bosi wake bila kupata ushirikiano.

Kwa mujibu wa Muriuki, madai ya kutaka kujiua hayana ukweli bali hizo ni njama zilizoibuliwa na polisi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles