26.1 C
Dar es Salaam
Friday, December 9, 2022

Contact us: [email protected]

Mgombea ubunge Bariadi ahaidi Neema kidato cha nne

Derick Milton, Simiyu

Mgombea ubunge jimbo la Bariadi Mkoani Simiyu kupitia Chama cha mapinduzi (CCM) Mhandisi Andrea Kundo amehaidi kuwasomesha wanafunzi wa kidato cha nne ambao watapata ufahulu wa daraja la kwanza alama saba na nane katika mtihani wa kitaifa mwaka huu.

Kundo amesema kuwa Mwanafunzi yeyote ambaye atapata ufahulu huo, atamsomesha kidato cha tano na sita hadi chuo kikuu na gharama zote za masomo zitakuwa juu yake.

Mgombea huyo ametoa ahadi hiyo wakati wa kampeini zake katika kata ya Ngulyati, ambapo ahadi mbele za wanafunzi wa shule ya sekondari inayomilikiwa na kanisa la Wasabato iliyoko kwenye kata hiyo.

” Mwanafunzi yeyote wawe wengi au mmoja, ambaye atapata ufahulu wa daraja la kwanza alama 7 na 8, gharama za kuendelea na masomoa hadi chuo kikuu, zitakuwa juu yangu,” amesema Mhandisi Kundo.

Aidha amesema kuwa endapo atachaguliwa atahakikisha anaboresha sekta ya Elimu katika Wilaya hiyo, ikiwemo kuboresha miundombinu yake ili kuwa rafiki kwa wanafunzi na walimu.

Akiongea katika mkutano wa hadhara na wananchi wa kata hiyo, mhandisi Kundo amehaidi kutengeneza Barabara kutoka kwenye kata hiyo hadi makao makuu ya Wilaya kupitia kijiji cha Ditima.

” Kwa muda mrefu wananchi wa huku wamekuwa wakiteseka kwenda makao makuu ya halmashauri wanalazimika kupitia Bariadi mjini, kutokana na Barabara hii kutopitika, nichagueni Mimi itapitika muda wote,” Amesema Kundo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,735FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles