27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mgombea huru Iraq ruksa

BAGHDAD, IRAQ

Rais wa Irag mapema jana ameridhia sheria mpya ya uchaguzi ambayo itatoa ruhusa kwa wagombea huru kushinda nafasi za ubunge, ikiwa hatua ya kuweka mambo sawa kuelekea uchaguzi wa mapema mwakani.

Rais Barham Saleh alisisitiza uhitaji wa uchaguzi huru, wa haki na uwazi katika zoezi la kuhesabu kura kwa lengo la kuwajengea imani wananchi wa taifa hilo katika mchakato mzima wa uchaguzi.

Sheria mpya imebadili majimbo 18 ya uchaguzi ambayo yalikuwa yakitumika awali, kuwa wilaya na kuvizua vyama kushiriki pasipo na upinzani katika maeneo hayo ambapo ilivisaidia kunyikulia viti vyote vya ubunge katika maeneo fulani, fulani.

Kwa hivyo sasa kura anaweza kupigiwa yeyote mshiriki katika kinyang’anyiro cha wilaya. Mabadiliko hayo ni muhimu kwa kuleta utulivu nchini Iraq na hasa Baghdad, ambayo ilikumbwa na maandamano mwaka uliopita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles