26.6 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

MGODI WA DHAHABU WA GEITA (GGM) WAKABIDHI MADAWATI 10,000 MKOANI GEITA

md-shanking-hands-with-students
Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM) Bw Terry Mulpeter akishikana mkono na mwanafunzi akiwa na mkuu wa Wilaya ya Geita Mh Hermani Kapufi pamoja na baadhi ya wanafunzi, wakifurahia baadhi ya madawati mapya ikiwa ni sehemu ya Madawati Elfu Kumi yaliyotolewa na mgodi wa GGM.

Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM) umetumia Jumla ya Shilingi 750 Milioni kutengeneza madawati 10,000 ambayo yamekabidhiwa rasmi jana Mkoani Geita kwa ofisi ya mkuu wa mkoa iliyagawanywa katika Wilaya Tano za Mkoa wa Geita.

Akipokea Madawati hayo kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mkuu wa Wilaya ya Geita Mh Herman Kapufi amesema kuwa Mkoa wa Geita umeshukuru kwa msaada wa madawati hayo kutoka kwa mdau wa maendeleo –GGM. “Tunapenda kushukuru kwa mchango huu wa madawati, lakini pia kutambua jitihada nyingine za kimaendeleo zinazofanywa na mgodi wa GGM. Ni jambo jema kuongeza kwamba kwa misaada hii, mkoa wetu tunatarajia utaendelea kufanya vyema katika sekta ya elimu kwa kuwa ufaulu wa wanafunzi kwenye Shule za Msingi umeanza kuimarika”

Akielezea uhaba wa madawati katika Halmashauri mbili za Mjina Wilaya ya Geita, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mjiwa Geita Bi Modest Apolinary amesema kuwa mchango huo ni muhimu sana katika kuboresha elimu kwenye Halmashauri za Wilaya na Mjiwa Geita.

“Halmashauri ya Mjiwa Geita ilikuwa na upungufu wa madawati 11,773 wakati yaliyopo ni 13,609 huku mahitaji ya kiwani 25,190, wakati houhuo halmashauri ya Wilaya ya Geita ilikuwa na upungufu wa madawati 22,066 lakini yaliyopo ni 33,514 wakati mahitaji ni 55,580.Kwa hiyo upungufu kwa Halmashauri zote ni madawti 33,839 lakini madawati yaliyopo ni 47,123 mahitaji yakiwa 80,770” alisema Bi Apolinary.

school-desk-donation
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mseto iliyopo Mkoani Geita wakifurahia madawati yaliyochangiwa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita.

 

Akizungumza na vyombo vya habari kwenye tukio hilo lililofanyika kwenye Halmashauri ya Mjiwa Geita, Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM) Bw Terry Mulpeter amesema GGM, kama jirani mwema, imeguswa na upungufu wa madawati mkoani Geita na ndiyo sababu imeamua kutengeneza madawati ili kuunga mkono jitihada za serikali katika kupunguza tatizo hilo hapa nchini.

Bw Mulpeter amesema Kampuni yake itaendelea kuchangia elimu Mkoani Geita ili kuleta maendeleo kwa kuwa elimu ndiyo msingi mkuu wa mabadiliko na maendeleo katika Jamii yoyote duniani. “Tumekwishatumia Bilioni Kumi za Kitanzania kujenga Sekondari ya kisasa ya Sayansi ya Nyankumbu  kwa ajili ya Wasichana zaidi ya 800 watakaokaa bwenini Mkoani Geita,Tumejenga pia Maabara na Maktaba za Kisasa kwa ajili ya kusaidia wanafunzi wa Kike katika masomo yao ya Sayansi, Hivi karibuni pia tumetoa Saruji na vifaa mbalimbali vya ujenzi kupunguza tatizo la madarasa na matundu ya vyoo kwenye shule ya Msingi Nungwena Nsanza zilizopo nje kidogo ya mjiwa Geita. Zote hizi ni jitihada za kuleta maendeleo katika jamii inayotuzunguka kupitia sekta ya elimu” Alisema Bw Mulpeter.

Bw Mulpeter alisisitiza kuwa elimu ni mojawapo ya haki muhimu za binadamu na kwamba elimu ni jambo muhimu kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu “GGM inaamini kuwa kuweka mazingira bora yakusomea ili watoto wetu wengi wahitimu vyema elimu ya msingi na sekondari na kuendelea na masomo ya juu itakuwa chachu ya maendeleo la taifa letu”

Akitoa neno la Shukrani kwa niaba ya Walimu wa Shule zilizoko Mkoani Geita, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mseto Bi Grace Ndimuhele amesema kuwa Shule yake ina wanafunzi 1266 lakini madawati yaliyopo ni 133 tu hivyo Mchango huo wa madawati elfu kumi Mkoani Geita, utaisaidia Shule hiyo kupata madawati ambayo yatapunguza tatizo la uhaba wa madawati yanayohitajika. Bi Grace ameongeza kuwa madawati yaliyochangiwa na Mgodiwa GGM yatapelekwa kwa wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili ambao wamekuwa wakikaa chini hali ambayo huathiri afya zao kutokana na mavumbi na uchafu.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mh Kapufi aliwaomba wadau wa maendeleo waendelee kuchangia mahitaji mbalimbali ya elimu mkoani humo

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles